BONGO MOVIE BADILIKENI, SOKO LISHAWACHOKA. - teknomovies
BONGO MOVIE BADILIKENI, SOKO LISHAWACHOKA.

BONGO MOVIE BADILIKENI, SOKO LISHAWACHOKA.

Share This
Washkaji uvumilivu umenishinda, hata salamu sitoi mana hili povu limenifika hapa….!!!, hakuna namna lazima nilimwage nimevumilia vya kutosha sasa nasema basi, chaguzi ni moja tu kumeza ama kutema. Povu hili linawahusu hawa wasanii wetu wa filamu wanaojiita Bongo Movie, mnivumilie tu mana lugha nitakayotumia humu inachoma kama pasi.





Kwanza ni ukweli ulio wazi wengi wenu mnafanya hii kazi kijanja janja yani hamkwenda shule, wengi wenu mmejifunza kudirect movie kupitia mafunzo (Tutorial) ya mitandao hasa hasa Youtube. Lakini kujifunza kwenye mitandao sio shida, shida ni kwa nini sio wabunifu kwenye kazi zenu? Kila siku tunaona yale yale kwenye movie kwa nini lakini? Mnaboa sana.

Tuanze tu na utengenezaji wa cover na kile kilichomo ndani (content) yani haviendani kabisa….narudia tena haviendani kabisa, picha zinazowekwa kwenye cover zinaonesha ni dhahiri imetokana na matwaka ya mpiga picha na si kama movie yenyewe inavyotaka. Jifunzeni basi hata kwa wenzenu hapo Nigeria namna ya utengenezaji wa cover “Art of Direction &Photography”.



Kiuhalisia cover inatakiwa isadifu kile kilichomo ndani yani content ya movie iendane na cover yenyewe lakini nyinyi sasa doooooooh.....!!!!! mnatuwekea color glade kibao halafu mnatafuta warembo wawili wanatabasamu na jana dume moja kawashika kiuno na ukiangalia movie inaitwa “Maisha ni Safari” na humo ndani huyo kijana ndo anahangaika kutafuta maisha, sasa unajiuliza kulikuwa na haja ya kuweka wanawake wawili kushikwa viuno? Mnaboa jamani.

Achana na hilo la Cover njoo kwenye story yenyewe ya movie, kila movie kijana anaetaka kufanikiwa basi lazima akatafute maisha mjini, hivi ni kweli mmeshindwa kutuaminisha kuwa hata kijijini mtu anaweza kufanikiwa? Mnakariri.

Movie inaitwa hukumu ya Ndoa yangu lakini hao wahusika (Bila shaka ndo wanandoa) wanacheka, hivi kuna hukumu inayofurahisha?
Ngoja niwashauri basi inatakiwa cover itokane na scenes za movie husika, yaani anaetayarisha some frames na kuziedit kuproduce cover, kama itahusisha thirdy party photographies ni sawa lakini iwe kidogo na sisi tusijue kuwa hii picha ilipigwa kwa kujitegemea, angalia makasha ya movie za nje ndo utaelewa ninachomaanisha...sio attention fake za mapendekezo ya mpiga picha ati kwamba "kumbatianeni, kaa chini ufanye kama unamuomba msamaha, kunja sura...Hapana , ukichukua picha za kwenye movie husika ndio zitakuwa na ile uhusika wa tukio halisi. Producers najua wanalijua hili, lakini kwanini hawafanyi hivyo? nahisi ni kwasababau ya low quality cameras wanazotumia, zile stills hazitakuwa HD. 


Basi nawashauri elimisheni madesigner wenu namna ya kuproduce film covers/posters zenye uhalisia wa maudhui ya filamu husika, sio kwenye kasha la CD naona choppers na milipuko ya mabumo wakati ndani ya movie sioni bullet hata moja isipokuwa milio tu ya risasi, acheni kuibia halaiki kwa kuuza "polished CD covers" wakati movie hata 720p haifiki...achilia mbali 1080p au vitu vidogo vidogo kama Sound editing, Color grading na Visual effects.

Mkiendelea hivyo bongo movie haivuki border nawaambieni. Jifunzeni kwa Bongo fleva. Msizalishe kazi kama njugu bila kuzingatia ubora wa vitu kama hivi maadamu mpate hizo ngawira za Steps Entertainment eti kwasababu Marketing chain inazunguka...hiyo marketing chain inayowapatia hela ya kula ya uhakika ni ile "low profile individuals" accross the country maana mtu anayejitambua hawezi hata kutazama hizo movie zenu, achilia mbali kuinunua kwa buku.

Mnisamehe kwa povu langu lakini mbadilike.

Usisahau kutu follow instagram na Twitter @TeknoMovies kwa update mbalimbali za movies na music.

No comments:

Post a Comment

Pages