The Fate Of The Furious Yaweka Record Hii Hapa - teknomovies
The Fate Of The Furious Yaweka Record Hii Hapa

The Fate Of The Furious Yaweka Record Hii Hapa

Share This
Filamu ya kampuni ya Universal Pictures‘ The Fate of the Furious imevunja rekodi kwakuwa na ufunguzi mkubwa zaidi wa muda wote baada ya kuingiza dola milioni 532 kwenye majumba ya sinema duniani mwishoni mwa wiki.


Kiasi hicho ni $98.8m toka Marekani na Canada $433.2m toka nchi zingine 63 mwishoni mwa wiki. Rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Star Wars: The Force Awakens iliyoingiza $529m.
The Fate of the Furious imeifanya Universal ifikishe dola bilioni 1 za makusanyo ya kimataifa ya filamu zake Ijumaa hii. Filamu hiyo imeingiza mkwanja wa kutosha kutoka Argentina, Colombia, Egypt, Estonia, India, Indonesia, Israel, Lebanon, Malaysia, Middle East, Pakistan, Panama, Paraguay, Peru, Portugal, South Africa, U.A.E., Uruguay, Venezuela, Belgium, Bolivia, Brazil, China, Denmark, Ecuador, Israel, na Mexico, Croatia, Czech Republic, Hong Kong, Iceland, Korea, Lithuania, Slovakia, Ukraine, U.K. na Ireland.
China pekee, ndani ya siku 3, filamu hiyo imeingiza $192.1m, kiasi ambacho hakijawahi kutokea nchini humo kwa filamu ya Hollywood.

No comments:

Post a Comment

Pages