Sio Muda Viongozi Wa Makundi WhatsApp Watapewa Uwezo Mkubwa Zaidi - teknomovies
Sio Muda Viongozi Wa Makundi WhatsApp Watapewa Uwezo Mkubwa Zaidi

Sio Muda Viongozi Wa Makundi WhatsApp Watapewa Uwezo Mkubwa Zaidi

Share This
WhatsApp wanaendelea kuiboresha App yao ambapo safari hii unaambiwa wanampango kabisa wa kuwaongezea nguvu Viongozi wa makundi (Group Admins)
Uwezo huo mpya ambao unatazamiwa kuja hivi karibuni, Utampa nguvu admin ya kuamua kuruhusu ujumbe fulani katika Group au kuondoa ujumbe pindi atapoona haufai katika Group.
Kipengele hicho kimeombwa kwa muda mrefu na watumiaji wengi wa mtandao huo na tayari katika baadhi ya nchi watumiaji wa WhatsApp Beta washaanza kufurahia huduma Hiyo.

SOMA PIA: FAHAMU NAMNA YA KUFUTA KABISA AKAUNTI YA WHATSAPP

Kuongezeka kwa nguvu hiyo kwa viongozi wa makundi kutasaidia kwa hali ya juu kupunguza taarifa za uongo na za uchochezi ambazo mara kwa mara zimekuwa zikisambazwa katika magroup mbalimbali ya WhatsAPP.

Tupe maoni Yako kuhusu Hili unafikiri Kutoa Uwezo huo hakutaweza Kudidimiza uhuru wa watumiaji wake? 

Source: teknokona pamoja na picha.


1 comment:

  1. Washindwe ktk jina la caballo 😢😢😢😢😢😢😢

    ReplyDelete

Pages