Filamu Tano Bora Kwa Mwaka 2017, Uchambuzi - teknomovies
Filamu Tano Bora Kwa Mwaka 2017, Uchambuzi

Filamu Tano Bora Kwa Mwaka 2017, Uchambuzi

Share This
Mwaka 2017 zimetoka Filamu nyingi kama kawaida ya wenzetu wazungu Ratiba nzima ya Ujio wa Filamu huwa inafahamika kwa Ufasaha na kila Filamu imetoka kutokana na Siku maalumu iliyopangiliwa.
Kuna utofauti kati ya Filamu Bora na Kali, Filamu inaweza kuwa Kali lakini isiwe Bora haha...Nisiwachanganye sana hapa leo nawaletea Filamu Bora kwa mwaka 2017 katika zile nilizotazama Mimi Binafsi naimani kila mmoja anaweza kuwa na Listi yake kutokana na Jinsi alivyotama Filamu Kwa mwaka Huu.

Nimetazama Filamu Nyingi sana Kwa mwaka 2017, Lakini hizi kwa mimi niliona kuwa na utofauti kidogo tofauti na nyingi.

Hapa nime Base upande wa Filamu za Mapigano Tu (Action) na Zipo kama Ifuatavyo.

5. SpiderMan:Homecoming
Inakuwa ni Filamu ya tatu Kutoka tangu waifanyie Kuirudia kiupya zaidi ambapo mbili zilizotangulia zilipewa Jina la The Amaizing SpiderMan ambazo alicheza mtaalamu Andrew Garfield.

Andrew Garfield
 Hii alipewa kazi Dogo Tom Holland ambae kwa hakika kwangu naweza kukiri kuwa ni mojawapo wa SpiderMan Bora kuwahi kutokea katika wote waliowahi kucheza Filamu hizo.

Tom Holland
Ubora wake zaidi kwa mimi nilichopenda ni kwa jinsi alivyoweza kubeba Ile uhusika wa kukufanya Ufurahi zaidi. Kitu poa zaidi ni kuonekana kwa Iron Man ndani Mr Tony Stark nacho kilikuwa ni kitu bora lakini cha zaidi ni namna Suti yake SpiderMan katika Filamu Hii Ilivyoboreshwa zaidi.

PITA HAPA PIA>>PAKUA SPIDERMAN HOMECOMING

Iliachiwa rasmi July 7 ambapo Mauzo ilifanya Poa sana ikikusanya mtonyo wa Dola Milioni $880.2 Kutoka bajeti ya Dola milioni $175.

Kwa mimi Hii naipa namba tano.

4. American Assasins

Filamu nyingine ni hii ambayo ilinishangaza hasa baada ya kumuona mtu mzima Dylan O'brien akibadirika na kucheza serious zaidi. Wengi tulizoea kumuona katika Role akipewa za kuchekesha kidogo mfano katika Series ya Teen Wolf lakini humu alizidi kudhihirisha kuwa yeye ni Noma na ni Jicho kubwa la baadae kutoka Hollywood.


PITA HAPA>>PAKUA AMERICAN ASSASINS

Ubora wa Hii filamu upo hasa kuanzia Stori kimtindo na Action zake, Ambapo Dylan alijitahidi vyema sana na kuleta Picha kuwa Bora haswa.

3. Overdrive


Wengi hawaijui Hii lakini kama Umepata nafasi ya kuitazama basi utakauwa Umekiri kuwa ni mojawapo ya filamu moja kali sana wengi wanaifananisha na Fast N Furiuos,

Scott Eastwood
Haijapata mafanikio makubwa sokoni lakini kwa kazi ambayo Scott Eastwood kaifanya ni hatari sana Huyu, Wengi mlimuona katika The Fast N Furious 8 .

PITA HAPA: BONYEZA HAPA KUPAKUA OVERDRIVE

Ubora wa hii kitu ni kuwa utapoanza kutazama, Hata kwenda kuchukua maji itakuwa ni ngumu sana mana Utafurahi na kila mara utakuwa unatamani ujue kipi kinachofuata ili uendelee kupata Burudani zaidi.

2. Hitmans Bodyguard 


Ubora wa Ryan Reynolds unazidi kukua zaidi na zaidi kila Filamu ambayo utamkuta basi lazima Ufurahi.

PITA HAPA>>PAKUA HITMANS BODYGUARD SASA

Sasa humu wakakutana na Samuel L Jackson wakatengeneza kitu poa sana, Sitoshangaa kusikia hii inakuja Sehemu ya Pili maana ya kwanza Jamaa wamekuwa na muungano mzuri sana na zaidi uwepo wa Mapigano ya hatari huku Ukiendelea kufurahi ni kitu ambacho kinaongeza utamu zaidi wa Filamu Hii.

Hapa naipa Namba 2 Kwangu.

1. John Wick:Chapter 2
Kama Ulitazama John Wick Ya kwanza ilitoka mwaka 2014, Mwaka huu wakatuletea muendelezo wa Pili. Ni bonge moja la Filamu ambalo kama mpaka sasa bado hujatazama Wewe mpenzi wa Filamu basi utakuwa umekosa mengi sana sana.

PITA HAPA PIA>>BONYEZA HAPA KUPAKUA JOHN WICK:CHAPTER 2

Napenda namna, JOHN anavyoichezea Silaha anavyotaka lakini ya Safari hii ilikuwa na moto zaidi tofauti na Mwanzo ambapo hii nayo sitashangaa kusikia Inakuja Sehemu ya Tatu maana hata mwisho wake kwa waliotazama watakuwa wameuona.

Tuachie maoni yako,Ipi unafikiri kwako ni Filamu Bora kwa mwaka 2017? Na kwanini umeichagua hiyo?Tumeanza na upande wa Mapigano Kuwa nasi Tutakuja pia na Filamu za Upande Mwingine Bora kama Za Kutisha N.K


No comments:

Post a Comment

Pages