WhatsApp Mabadiliko Mapya Video Na Voice Notes,Fahamu - teknomovies
WhatsApp Mabadiliko Mapya Video Na Voice Notes,Fahamu

WhatsApp Mabadiliko Mapya Video Na Voice Notes,Fahamu

Share This
WhatsApp kama kawaida wameendelea kuboresha App yao ambapo safari hii wameleta uwezo mpya ambapo mtu ataweza kutazama Video moja kwa moja kupitia WhatsApp na si kwenda sehemu nyingine.
Kwa kawaida imekuwa mfano mtu akiweka Linki ya Youtube katika WhatsApp na kubonyeza humpeleka eneo lingine katika App ya Youtube Lakini kwa sasa mtu ataweza kutazama moja kwa moja kwenye App hiyo.

SOMA PIA:FILAMU BORA KWA MWAKA 2017

Ukiachana na Hilo pia unaambiwa wanakuja na Uwezo mwingine ambapo mtu kwa mfano anapokuwa anarekodi voice note ilikuwa inambidi kushikilia kitufe cha Voice note lakini katika mabadiriko mapya kutakuwa hakuna tena uwezo wa kuweza kushikilia mpaka kumaliza ujumbe wako bali utabonyeza tu na kurekodi sauti yako.

Mabadiriko haya wameanza kuyapata tayari watu wanaotumia simu za Iphone ambazo zinatumia mfumo endeshaji wa Ios lakini inataarifiwa kuwa sio muda watumiaji wote wataanza kufurahia uwezo huo.

Source: teknokona pamoja na picha.

No comments:

Post a Comment

Pages