BOSS MWINGINE TENA HOLLYWOOD KITANZINI KWA KASHFA YA NGONO - teknomovies
BOSS MWINGINE TENA HOLLYWOOD  KITANZINI KWA KASHFA YA NGONO

BOSS MWINGINE TENA HOLLYWOOD KITANZINI KWA KASHFA YA NGONO

Share This
Operesheni ya kufichua maovu wanayofanyiwa waigizaji wa kike Hollywood inaendelea kushika kasi huku Director James Toback nae akishutumiwa juu ya unyanyasaji wa kingono kwa waigizaji wa kike.
Toback ameshutumiwa katika mtandao wa Twitter baada ya Superstars wa kike wa Hollywood kuanzisha kampeni maalum ya kufichua uovu wote wanaofanyiwa yenye hashtag ya MeToo(#MeToo) ambapo jamaa ametajwa kuwa amewanyanyasa kingono zaidi ya wanawake 38.

SOMA PIA : BOSI WA AMAZON KITANZINI KWA KASHFA YA NGONO

Director James mwenye umri wa miaka 72 amewahi kuongoza filamu nyingi lakini zilizompa umaarufu ni “Bugsby”na “Two Girls and a Guy” ambazo filamu hizo zinadaiwa kutumika kama mbinu ya kuwanasa wanawake ambao walishiriki kwenye movie hizo.

SOMA PIA : LUPITA NAE AMWAGA UCHAFU WA BOSS HOLLYWOOD KUMNYANYASA KINGONO

Mwingizaji wa kike Rinaldi amefunguka namna walivyokutana na Director James

Rinald aliandika
Siku zote anataka nifuate maelekezo nikiwa hotelini au niende nyumbani kwake sasa nikawa nashangaa huyu mtu ananiambia nini? Kwa akili ya kawaida nilijua kuwa hiki ni kipimo kama mimi ni msanii wa kweli na nina shauku ya kuigiza
Nae mwimbaji na mpiga gitaa  Veruca Salt amesema
Hana kingine anachopenda zaidi ya kujichua huku akiniangalia usoni 
Sari Kamin ambae ni mtangazaji wa radio aliliambia jarida la Medium kuwa alikutana na Toback mwaka 2003 baada ya kushawishiwa na Director huyo kuigiza kwenye moja ya kipande cha movie na kwa kuwa yeye anapenda kuigiza alikubali na hivyo kukutana nae hotelini.
Hakutaka kutushirikisha kwenye movie, alitumia njia hiyo kutulaghai na kutudhalilisha kwa kuwa yeye ni maarufu basi alidhani tungebaki kimya, lakini muda wa kukaa kimya umekwisha.
 Toback amepokea malalamiko hayo huku akisema yeye hausiki na kama angekuwa muhusika basi angatajwa miaka hiyo ambayo ameshutumiwa kufanya uchafu huo

Wasanii wengine wametumia uwanja huo wa Twitter kuonyesha machukizo yao juu matendo hayo ya waandaaji wa Filamu.








Usisahau Kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Updates mbalimbali lakini pia Subscribe Youtube Channel ya DM Online Tv.


Pages