Aliyeandika 'Good Morning' kwa kiarabu akamatwa na polisi kwa uchochezi - teknomovies
Aliyeandika 'Good Morning' kwa kiarabu akamatwa na polisi kwa uchochezi

Aliyeandika 'Good Morning' kwa kiarabu akamatwa na polisi kwa uchochezi

Share This
Polisi nchini Israel imemkamata kijana mmoja mwenye asili ya Palestina kwa kosa la kuandika "Good Morning" kwa kiarabu kwenye mtandao wa Facebook.

Kijana huyo ambae jina lake limehifadhiwa amekamatwa na Polisi baada mtandao wa Facebook kushindwa kutafsiri neno la Kiarabu la Asubuhi Njema na kutafsirika "Washambulie hao" kwa lugha ya Kiyahudi.
Kwa mujibu wa maelezo ya polisi kutoka Judea na Samaria nchini Israel inaeleza kuwa  kijana huyo ni mfanyakazi wa kampuni ya ujenzi na aliposti picha hiyo akiwa katika maeneo ya West Bank.

Polisi wameeleza kuwa baada ya kuona posti hiyo walichukua uamuzi wa kumsaka kijana huyo na kumkamata ndani ya masaa matatu ili kumuhoji kuhusu kauli yake iliyotafsiriwa kama ni ya kichochezi.

SOMA PIA:MAKALA KUMUHUSU ROSA REE

Hata hivyo masaa machache baada ya mahojiano aliachiwa huru na polisi baada ya kupata msaada kutoka kwa mtalaamu wa Lugha aliyetafsiri kwa ufasaha neno hilo la ‘Goood Morning’ kwa lugha ya kiyahudi.

Facebook imekuwa ikilaumiwa na watu wengi wanaotumia lugha mbalimbali duniani kwa kushindwa kutafsiri kwa ufasaha baadhi ya maneno kutoka kwenye lugha husika.

Kwa upande mwingine Polisi wamesema walipatwa na hofu kubwa kwa kumuona kijana mwenye asili ya Palestina akiandika ujumbe huo uliokaa kichochezi huku akiwa karibu na Tinga Tinga.

 Ambapo eneo hilo hilo miezi miwili iliyopita kulitokea tukio la kigaidi baada ya watu waliosadikika kuwa ni magaidi waliendesha Tinga Tinga kwenye umati wa watu na kujeruhi watu wawili.

Nchini Israel hakuna polisi wa kutosha wanaojua kiarabu kwa ufasaha hivyo mara nyingi matatizo kama hayo hutokea.

Source: Csoonline.com

Usisahau Kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Updates mbalimbali lakini pia Subscribe Youtube Channel ya DM Online Tv.

Pages