Filamu Zilizouza Zaidi Kuzidi Nyingine Kwa Muda Wote-Hollywood - teknomovies
Filamu Zilizouza Zaidi Kuzidi Nyingine Kwa Muda Wote-Hollywood

Filamu Zilizouza Zaidi Kuzidi Nyingine Kwa Muda Wote-Hollywood

Share This
Kwa wenzetu nje mauzo yao ya filamu yanatokea kwenye vyanzo kama zinduzi mbalimbali katika masinema,Kuonesha katika luninga,na pia kwa mauzo mbalimbali ya Cds.

Filamu za kivita,Muziki na pia filamu za historia katika list ya filamu zinazokimbiza zaidi kimauzo zimekuwa zikifanya vizuri na hata katika List ya Filamu zilizouza zaidi kwa muda wote utaziona za kutosha.

Filamu kama za mfululizo Star Wars,Harry Potter,Pirates of Carribean bila kusahau Filamu za Ma Super Heroes kama X-Men,Spiderman na zingine bado zinaendelea kuuza zaidi.
Huwezi kuacha kuzitaja filamu pia za Animations kama,Despicable Me,The Lion King,Finding Nemo,Zootopia ambazo nazo kila mara zinapoachiwa zimekuwa zikifanya vizuri nyingi zikitoka kwa ndugu zetu Disney ambao wanasifika kwa kutengeneza Animation Kali sana.

Filamu mpaka sasa ambayo imeweza kuuza zaidi kuliko zingine zote ni Avatar ambayo imeweza kuuza mpaka sasa Bilioni $2.7 ambayo ni sawa na Trilioni 6.2 Kwa kibongo Bongo.

Lakini wanasema mpunga unaweza kuzidi zaidi kama wataingiza mauzo ya Cds na pia maonesho katika Luninga lakini,huwa hawapendi kutumika rekodi hizo kwa sababu huwa zinachanganya katika kujua ukweli halisi.

Filamu ya pili ni Titanic ambayo mpaka sasa imeweza kuuza Dola milioni $2.1 ambazo ni sawa na Trilioni 4.9 za Kitanzania. Lakini kwa upande wa Titanic,Mauzo yake mengi yametokea katika mauzo ya Cds.

Unaweza ukatazama hapa Chini List Ya Filamu Jinsi Zilivyopangwa kuanzia ya Kwanza mpaka Ya 10,Fanya Kuibonyeza Picha ili Uweze Kuiona Vyema au bonyeza HAPA kutazama List Nzima Ya Filamu 50.
List Ya Filamu Zilizouza Zaidi Kwa Muda Wote Mpaka Sasa Katika Top Ten














Pages