DARREN SHAHLAVI MTU HATARI ALIYEACHA SIMANZI. - teknomovies
DARREN SHAHLAVI MTU HATARI ALIYEACHA SIMANZI.

DARREN SHAHLAVI MTU HATARI ALIYEACHA SIMANZI.

Share This

Wazazi Wake Wote Wawili Walikua Ni Wazaliwa Halisi Kutoka Iran Ambao Walihamia England Na Kuweka Makazi Hapo Ambapo Kijana Huyu Alizaliwa. 

Darren Shahlavi Alizaliwa Tarehe 5 August Mwaka 1972 Huko Stockport, Cheshire England. 

Akiwa Na Miaka 7 Alianza Kujifunza mchezo wa Judo Katika Jumba La Maigizo Ambapo Alikua Akiwahi Asubuhi Na Mapema Na Kuanza Kuwaangalia Kwanza Waigizaji Mbalimbali Wakifanya Yao. 

Baada Ya Kutazama Baadhi ya Filamu Za Bruce Lee Na Jackie Chan Alijikuta Akitamani Kuja Kua Bonge La Mwigizaji Na Ndo Ndoto Yake Ilianzia Hapo. 

Alipofikisha Miaka 14 Alianza Kujifunza Boxing Na Kickboxing Na Pia Shotokan Karate Na Alipotimiza Miaka 16 Aliamua Kuingia Rasmi Sasa Katika Maswala Ya Uigizaji Ambapo Alisafiri Kwenda Hong Kong Ili Kuanza Safari Yake Hiyo. 


Yuen Woo-ping Director Na Pia Action Choreagrapher Alimuona Jamaa Kua Anaweza Ambapo Alimuweka Katika Filamu Yake Ya Tai chi Boxer Ambapo Alicheza Na Star Jacky Wu. 

Kwa Muda Huo Bado Alikua Pia Akifanya Kazi Kama Bouncer Katika Night Club Na Pia Kama Mlinzi Wa Mastar Wa Kigeni. 

Nyota Yake Ilianza Kuonekana Hapa Baada Ya Kucheza Kama Jambalika Katika Mchongo Huu BLOODMON hiyo Ilikua Mwaka 1997.

Ukiachana Na Uigizaji Jamaa Pia Alikua Na Uwezo Wa Kufanya, Tunaita Stunt Yani Action Ambazo Kiuhalisia Ni Kazi Kufanyika Au Sometimes Actors Wenyewe Kuna Action Huwa Wanazishindwa Hivo Hawa Ndo Huwa Kazi Yao Tunaita Ma Stuntsmen Ambapo Hiyo Kazi Aliipiga Katika Baadhi Ya Movie Kama The Chronicles Of Riddick, Night At Museum Na Warnet Bros 300.

Mwaka 2010 Alizidi Kung'aa Baada Ya Kucheza Katika Movie Ya Ip man 2 Ambapo Fighting Scenes Zake Zilipendeza Haswaa. 

Pia Kuna Filamu Kadha Wa Kadha Alitokea Kama.. 
Red Riding Hood
Mortal Combat:Legacy 
The Package
The Marine 3
In The Name Of The King
Blood Rayne 
300
Watchmen N.K

Katika Maisha Yake Binafsi Alimuoa Mwanadada Bondia Kutoka Canada Akifahamika Kwa Jina La Luraina understute Mwaka 2000 Na Mwaka 2003 Waliachana Wakiwa Hawajapata Hata Mtoto Mmoja. 


Mwaka 2015 Tarehe 14 January Jamaa Alifariki Akiwa Usingizini Na chanzo Cha Kifo Baadae Ilifahamika Kua Ni Shambulizi La Moyo

  Chini Nimekuwekea Video Ya Baadhi Ya Scenes zake za Mapigano Yake Bora,Tazama Sasa.

            

Pages