DADA AITA POLISI KUMPA KICHAPO KAKA YAKE, KISA? - teknomovies
DADA AITA POLISI KUMPA KICHAPO KAKA YAKE, KISA?

DADA AITA POLISI KUMPA KICHAPO KAKA YAKE, KISA?

Share This
Kwa mujibu wa ripoti kutoka Nigeria, mwanadada tajiri nchini humo ameamua kutumia Polisi kumzuia Kaka yake asioe mwanamke ambae yuko nae kimahusiano takriban miaka 3.
Mwanadada huyo aliyetambulika kwa Jina la Ms Uzoma Umesi ambae ni mmiliki wa kampuni ya MBS iliyopo Ikoyi mjini Lagos aliamuru Polisi ambao amewaajiri katika moja ya kampuni yake ya Ulinzi waende kumpiga Kaka yake kwa sababu mwanamke aliyechagua kuoa haendani nae.

Dada huyo alipatwa na hasira kwani kila akimshauri kaka yake kumuacha mwanamke alikaidi ndipo akaamua kuchukua uamuzi huo.
Pamoja na kaka huyo Okechukwu Umesi kukumbana na kichapo kichapo hicho, bado mapenzi yake yako mubashara kwa mpenzi wake.

No comments:

Post a Comment

Pages