Mjue Mkali Wa Filamu Za Kibabe, Mattias Hues - teknomovies
Mjue Mkali Wa Filamu Za Kibabe, Mattias Hues

Mjue Mkali Wa Filamu Za Kibabe, Mattias Hues

Share This
Alifahamika Vilivyo Sana Pale Alipocheza Katika Movie Ya No Retreat No Surrender 2...Lakini Je Huyu Mtu Ni Nani Haswa? 

Ebu Acha Tumuangalie Kwa Ufupi Jina Lake Kamili Anaitwa Mattias Hues Amezaliwa February 14 Mwaka 1959 Huko Katika Kitongoji Cha Waltrop, Germany Lakini Kwa Nchi Zinazoruhusu Uraia Wa Nchi Mbili Jamaa Pia Ni Raia Wa Marekani Lakini Mpaka Sasa Anaishi Ujerumani. 

Baada Ya Kumaliza Shule Hues Alihamia Paris Ambako Alienda Kujifunza Mambo Ya Hotel Management. 

Akiwa Huko Alianza Kujishughulisha Na Mambo Ya Mazoezi Na Alijiunga Katika Baadhi Ya Club Za Kufanyia Mazoezi Ambapo Hiyo Ilimpa Motisha Zaidi Ambapo Aliporudi Germany Alifungua Club Mbili Za Mambo Ya Michezo. 

Baadae Alikuja Kuziuza Club Zake Hizo Na Kuamua Kutimkia Nchini Marekani Katika Jiji La California Ambapo Alijiunga Na Club Kubwa Ya Mambo Ya Mazoezi Na Pia Mafunzo Ya Utunishaji Misuli Inayofahamika Gold's gym. 

Akiwa Hapo Ndo Bahati Ilimdondokea Kivipi? Sikia Hii... 

Derek Barton Huyu Jamaa Alikua Ni Managing Director Wa Gym Hiyo  Pia Alikua Ni Stunt Man Katika Hollywood Alipokea Simu Kutoka Kwa Producer Wa Movie Ya No Retreat No Surrender Ambapo Alimwambia Kua Van Damme Kakataa Kucheza Movie Hiyo Hivyo Anatafuta Mtu Wa Kucover Nafasi Hiyo. 

Barton Alimchagua Hues Kwenda Kufanya Audition Kwaajili Ya Kushiriki Movie Hiyo Na Kweli Alifanikiwa Kupita Licha Ya Kwamba Hakuwahi Kufanya Movie Yoyote Ile Katika Maisha Yake. 

Hivyo No Retreat No Surrender 2 Ndiyo Iliyofungua Dira Kwake Ambapo Alipiga Mchongo Vyema Na Ndo Ukampa Deal Nyingine Pia Za Movies Mbali Mbali. 

No Retreat No Surrender 2 Ilitoka Mwaka 1987 Ikiwa Ndo Movie Yake Ya Kwanza Zikafuata Zingine Kama.. 

Dark Angel (1990)
Age of treason (1993)
Alone in the woods (1996)
Big Top pee-wee (1988)
Star Trek vi : The Undiscovered Country (1991)

Kwa Miaka Ya Karibuni Kacheza Pia Katika Baadhi Ya Movie Kama Show Down In Manila (2016)
The Sleeper, Deadly Recall (2012)
The Rogue (2009)
CarPirates (2008)
Goy (2008)
D-war (2007)

Matthias Ni Moja Kati Ya Watu Ambao Kutokana Na kukaa Nje Kwa Muda Kidogo Kapoteza Ile Lafudhi Ya Kijerumani Kabisa Yani Mpaka Watu Wengine Hupinga Kua Jamaa Sio Mjerumani. 

Ungana Nasi Twitter na Instagram @Teknomovies




Pages