AFUKUZWA SHULE KWA KUCHORA PICHA YA KUTISHA. - teknomovies
AFUKUZWA SHULE KWA KUCHORA PICHA YA KUTISHA.

AFUKUZWA SHULE KWA KUCHORA PICHA YA KUTISHA.

Share This
Mkurugenzi wa Elimu mkoani Nakuru nchini Kenya amemuamuru mkuu wa shule ya Bahati (Bahati Boys High school) kumrudisha shuleni mwanafunzi aliyefukuzwa kwa kosa la kuchora picha ya kutisha iliyotafsiriwa kama Alama ya mapepo.

Mwanafunzi huyo anayesoma kidato cha nne katika shule hiyo ya dini Ian Njenga, amefukuzwa shuleni hapo tarehe 13 february baada kuchora picha iliyotafsiriwa kama alama ya Freemason.

Mwalimu mkuu amesema si mara ya kwanza kijana huyo kuchora picha za ajabu, imekuwa ni desturi yake hivyo wanaamini kijana huyo huenda akawa ni freemason.

Hata hivyo mwalimu huyo amewasihi wazazi wa Ian wakae nae mtoto wamfanyie huduma ya counselling ili arudi katika hali ya kawaida kwani hufanya mambo ya ajabu shuleni.

No comments:

Post a Comment

Pages