Angelina Jolie Amekuja Na Dude Hili Hapa - teknomovies
Angelina Jolie Amekuja Na Dude Hili Hapa

Angelina Jolie Amekuja Na Dude Hili Hapa

Share This
BAADA ya kuachana na mme wake ambae waliweza kudumu kwa muda mrefu,Angelina Jolie kwa mwaka huu amerudi kivingine kwa kuweza kuleta filamu inayofahamika kwa jina la First They Killed My Father ikiwa ni stori ya maisha ya kweli.

Filamu hiyo ambayo imeongozwa na Angelina na pia akiwa kama Produza,imekuwa ni filamu ya kipekee ambayo imeongozwa na mtu kutoka Hollywood huku lugha ikitumiwa ya Cambodia ambapo ndipo stori ilipoakisiwa.
Kwa mara ya kwanza kiliandikwa kitabu na mwanamama Loung Ung ambae katika miaka ya 1975 mpaka 80 katika vita iliyotokea huko Cambodia aliweza kushuhudia mambo mengi ya hatari ambapo takribani wananchi wa Cambodia milioni moja walipoteza maisha.
Filamu hiyo imeachiwa Septemba 15 katika mtandao wa Netflix na imeweza kupata mafanikio makubwa huku wataalamu mbalimbali wa mambo ya filamu wameweza kusifia namna Angelina alivyoweza kuiongoza .

Katika moja ya mahojiano Angelina anasema, amefurahi kuweza kufanya kazi y filamu kama hiyo na kwake kaifanya kwa nguvu zote sababu ndicho kitu anachokipenda kufanya.

“Ni furaha kwangu kuweza kutoa nguvu zangu katika filamu hii na hakika mafanikio yanaonekana ,” alisema. 

Tazama Trailer hapa Chini kwa kubonyeza kitufe cha Play.....


            

No comments:

Post a Comment

Pages