Ali Kiba Atoa Neno Kuhusu Lissu - teknomovies
Ali Kiba Atoa Neno Kuhusu Lissu

Ali Kiba Atoa Neno Kuhusu Lissu

Share This
NAWEZA nikasema kwa mwaka huu mpaka unamalizika Ali Kiba hawezi kusahau mafanikio aliyopata kutokea wimbo wake wa Seduce Me ambapo ukiachana na kuweka rekodi kwa kutimiza watazamaji milioni 2 kwa masaa 38 na watu mbalimbali mashuhuri kutoa ya moyoni kuhusu wimbo huo na mmoja wapo alikuwa ni mbunge wa Singida.

Mbunge huyo ambae amelazwa Nairobi,Kenya Ali Kiba aliweza kutoa yake juu ya ishu ya mbunge Lissu ambae ni moja ya mfuasi wa wimbo wake wa Seduce Me.

“Namuombea kwa Allah tu,aweze kupona na kurudi katika hali yake ya kawaida sababu ni mtu ambae nilishangazwa sana na maoni yake juu ya wimbo wangu,hicho tu sina mengi ya kusema,”

Aidha pia Ali Kiba aliongeza juu ya watu wengine ambao waliweza kutoa maoni yao juu ya wimbo huo na kutukanwa kama mwimbaji wa injili Christina Shusho ambae alitukanwa sana baada ya kuweka maoni yake juu ya wimbo huo.


“Daah yani Dada wa watu hadi nilimuonea huruma nasikia alitukanwa sana,lakini natambua maoni yake juu yangu shukrani sana kwake,” alimaliza.

No comments:

Post a Comment

Pages