Madee:Nay Wa Mitego mtoto mdogo sana - teknomovies
Madee:Nay Wa Mitego mtoto mdogo sana

Madee:Nay Wa Mitego mtoto mdogo sana

Share This
PENGINE unaweza kufikiri bifu lao limeisha kutokana na wao wanavyodai lakini kutokana na maneno wanayoongea wote wawili hali inaonekana bado si nzuri.

Katika mahojiano na Mwanaspoti ,Madee aliulizwa juu ya bifu lao kama limeisha ama laah.
“Sina bifu na Nay na wala siwezi kuwa na bifu nae ni kutofautiana tu kauli lakini pia mi niwe na bifu na Nay,mbona mtoto mdogo sana kwangu,”

“Mimi wakati natoa wimbo wangu wa kwanza yeye sijui alikuwa yupo sekondari hata sijui , kwahiyo siwezi kuwa na bifu na mtoto mdogo kabisa,” Aliongeza.

Pia Madee alijibu shutuma ambayo imewahi kutolewa na Jackline Wolper juu ya video ya Sikila ambapo Wolper alidai Madee kutumia sura yake bila idhini yake.

“Unajua suala la katuni ni suala ambalo ni kama la kubuni tu,haimaanishi kwamba ndo sura halali ya mtu Fulani,sasa mimi nilishangaa kwa alichokisema lakini yote na yote nshukuru mambo yalienda safi,” aliongeza zaidi





No comments:

Post a Comment

Pages