Kevin Hart Kakiri Kuchepuka - teknomovies
Kevin Hart Kakiri Kuchepuka

Kevin Hart Kakiri Kuchepuka

Share This
MCHEKESHAJI na pia muigizaji nguli kutoka katika ardhi ya Rais Trump,Kelvin Hart ameamua kuweka wazi juu ya shutuma alizokuwa amezushiwa juu ya kumsaliti mke wa sasa anaefahamika kwa jina la Eniko Parrish ambae ni mjamzito kwa sasa.

Katika video aliyoweka katika mtandao wa Instagram Hart aliomba radhi na kusema yeye ni binadamu hivyo anaomba msamaha kwa kitendo hicho alichokifanya huku akitumia dakika moja ipasavyo kwa kumzungumzia mke wake na familia yake kiujumla.

““Niombe radhi kwa mke wangu, watoto wangu nimefanya makosa najua nilipitiwa na nikafanya ujinga huo, hilo kosa nilibebe mimi kweli nilifanya. Mimi ni binadamu daima sijakamilika, nilitegeka katika mazingira ambayo sikutarajia kufanya hivyo,“ alisema.

Hii si mara ya kwanza kwa Kelvin Hart kuchepuka kwani katika mahusiano yake ya awali na Torrei Hart chanzo cha kuachana ilifahamika kuwa ilikua ni kuchepuka na safari hii tena karudia tena kamchezo.


Mke wake wa sasa mpaka sasa bado hajatoa tamko lolote,hivyo hali imebaki katika sintofahamu juu ya mustakabali wa familia hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages