American Sniper, Stori Ya Kweli Isiyochosha - teknomovies
American Sniper, Stori Ya Kweli Isiyochosha

American Sniper, Stori Ya Kweli Isiyochosha

Share This
Kitu kimoja ninachokipenda kutoka katika Soko la Hollywood ni ubunifu mkubwa na uwezo wa kukiwasilisha kile wanachokusudia katika uhalisia mkubwa.

American Sniper rasmi iliachiwa tarehe 25 mwezi Desemba mwaka 2014. Filamu hii inahusu maisha ya ukweli kabisa ya mlenga shabaha maarufu Hayati Chris Kyle ambae aliandika kitabu kikifahamika kwa jina la American Sniper:The autobiography of the most Lethal Sniper In US Military History ambacho alikiachia mwaka 2012.

Ndani ya kitabu hicho, Chris alielezea maisha yake akipambana katika vita ya Iraq ambapo aliweza kuokoa maisha ya wanajeshi wenzake kutokana na shabaha zake za hatari.

Katika vita hiyo,wenzake na Chris walimpa jina la utani la “Mr Legend” sababu ya sifa yake kuu ya kuweza kulenga bila kukosa na inakadiriwa aliweza kuua zaidi ya magaidi 105 hiyo ni idadi inayofahamika rasmi ila inatazamiwa ni zaidi ya hapo.

Tumjue vizuri Chris Kylie.

Christopher Scott Kylie alikuwa ni mzaliwa kutoka kitongoji ch Odessa huko Texas na April 8 mwaka 1974 ndo siku ambayo alionja pumzi ya duniani kwa mara ya kwanza.
Katika jeshi alianza kazi rasmi mwaka 1999 mpaka mwaka 2009 ambapo aliweza kupambana vyema katika vita ya Marekani na Iraq katika Troops 4.

Kifo Chake.

Chris Kylie alifariki February 2 mwaka 2013 na kuzikwa huko Texas State Cemetery.

Chanzo cha kifo chake ilikua ni kupigwa na risasi ambapo alikuwa pamoja na rafiki yake,walipigwa risasi wote wakiwa katika eneo maalumu la kujifunzia kulenga shabaha na mtu aliyefanya jambo hilo alikuwa ni rafiki yao ambae alikuwa nae mwanajeshi ambae alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya akili, pamoja na stress ambapo Kylie pamoja na rafiki yake Chad Littlefield walikuwa wamemchukuwa na kumpeleka eneo hilo ili waweze kufurahi pamoja na kumtuliza mshikaji wao.

Lakini hali ikawa hali,Chris ndo ikawa siku ya maisha yake huku Jamaa aliesababisha tukio hilo mwaka 2015 alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

Turudi Kwenye Filamu.

Utapotazama filamu ya American Sniper mwishoni kuna Footage ambazo zinaonesha siku ya mazishi jinsi ilivyokuwa ambapo alizikwa kwa heshima ya hali ya juu na watu mbalimbali walitoa heshima zao njiani wakati gari likielekea katika maziko.

Chris aliacha mke, pamoja na watoto wawili ndivyo hata kwenye filamu utaona hivyo hivyo.

Kwanini Yakupasa Utazame Hii Filamu?

Filamu hii ilichukua tuzo ya Best Sound Editing. Na kweli naweza nikasema ilideserve sababu ndani sauti inasikika fresh bila mikwaruzo na hata risasi ikipigwa unaisikia vyema kabisa kama mtu unazijua vyema risasi basi hali hiyo utaifeel.

Haina Complication kubwa sana kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Haiihitaji kuumiza kichwa ili kuweza kuielewa. Huwa napenda kuongezea hapa hata ukiwa unachati huku unatazama huu mchongo utaelewa sawia kabisa.

Bradley Cooper ameweza kufanya kazi inavyotakiwa na kuzidi kudhihirisha kwamba yeye ni bora kwa kila idara.
Bradley Cooper
Hakikisha unapenda Filamu za walenga shabaha ndipo utaweza kufurahia zaidi hii filamu ambayo katika mitandao kadhaa baadhi ya maoni ya watu wameonesha kuiponda hasa kutokana na tabia ya Wamarekani kupenda kujivika Ushujaa kwa mambo mengi.

Zaidi na Zaidi inabidi upende filamu za kivita lakini kwa hii haihitaji sana kupenda filamu hizo sababu ya mtiririko uliopangwa vyema kwa stori murua inayo sadifu maisha halisi ya nje ya vita.

Kwa uliyetazama hii filamu hakika hautaacha kusema sehemu nzuri sana kama sehemu alipomlenga kwa shabaha kali moja ya Sniper aliyewasumbua sana tena kwa umbali mrefu sana.

Sitaki kuweka maneno mengi,Kama hujatazama hii kitu unaweza wasiliana na Mhariri mkuu ataekupa maelekezo ya kila namna jinsi ya kuipata filamu hii.


Usisahau kufuata katika Instagram na Twitter @Teknomovies.

Bonyeza Play Hapo Chini Kutazama Trailer Yake.
              

No comments:

Post a Comment

Pages