Mambo Kadha Usiyoyajua Kuhusu Uhusika Wa Tony Stark #Iron Man - teknomovies
Mambo Kadha Usiyoyajua Kuhusu Uhusika Wa Tony Stark #Iron Man

Mambo Kadha Usiyoyajua Kuhusu Uhusika Wa Tony Stark #Iron Man

Share This
Katika list ya Filamu zangu bora kwa upande wa sayansi za kufikilika (Science Fiction)  Iron Man ni filamu ambayo haiwezi kukosa katika list yangu.

Ubora wa filamu haufichiki hasa kutokana na ubora wa uhusika wa Tony Stark (Robert Downey Jr) ambae ameweza kuifanya filamu kuvutia sana.

Lakini kuna mengi watu huwa hawajui juu ya uhusika wa Tony Stark ambao umejengwa katika filamu ebu ngoja nikufahamishe fasta kuanzia kumi mpaka moja.

10. Ilichukua miaka 20 kufanyika kwa filamu ya kwanza ya Iron Man.

Kuanzia mwaka 1999 ndipo wazo la kufanyika kwa filamu lilipangwa lakini haikufanikiwa kufanyika. Tena mwaka 2001 mipango ilianza kufanyika lakini haikufanikiwa tena.
Inasemekana katika mipango hiyo waigizaji kama Tom Cruise na Nicolas Cage walikuwa wanategemewa kucheza kama Tony Stark.

9.  Ni moja ya waanzilishi wakubwa wa The Avengers.

Wengi mmetazama filamu hiyo ambayo imejaa watu hatari kama The Hulk,Captain America,Thor ambao kihistoria inaonesha kuwa mtu aliyeunganisha timu hiyo ni Tony.
Na hata makao makuu yao yalikuwa katika nyumba ya Tony,Usisahau kuwa Jamaa katika filamu ni moja ya mabilionea hatari na wanaopendwa na wengi hasa mabinti.

8.  Alifundishwa ngumi na Captain America.

Unaweza ukashangaa lakini huo ndo ukweli ki filamu filamu. Hili lilikuwa linafahamika wazi kuwa Tony bila kutumia suti yake kiuhalisia ni mtu wa kawaida tu. Lakini baada ya muunganiko wa Avengers alikuwa akifundishwa ngumi na Camptain mwenyewe kwamba endapo hali ikibadilika aweze kupambana hata bila kuwa na suti yake.

7.  Tony ana Masters degree ya mambo ya Fizikia pamoja na Engineering alipata akiwa na miaka 17 tu

Hiyo kifilamu filamu,Akiwa na miaka 16 alienda kusoma katika Massachusetts Institute of Technology na miaka miwili mbele alimaliza akiwa na master yote kutokana na U genius wake.

6. Anamiliki “Area 51”

Jamaa ni tajiri sana,hivyo aliamua kununua Area 51 ambayo  makazi kwa watu hayaruhusiwi na ni eneo kwaajili ya majaribio ya kijeshi. Hivyo yeye alinunua kwa shughuli zake mwenyewe japokuwa katika filamu hatujawahi kuoneshwa sana namna lilivyotumika

5. Ili Kujiandaa na role ya Iron Man, Robert Downey Jr alitumia siku tano kufanya mazoezi ya nguvu kwaajili ya kujiweka mwili wake fiti kwaajili ya role hiyo iliyomtaka kuwa na mwili stahiki kuendana na muhusika Tony

4. Iron Man ndio filamu pekee ya kwanza Marvel kutumia mpunga wao wenyewe bila kusaidiwa na kampuni nyingine yoyote.

3. Unaweza kutengeneza Suti ya Iron Man ukiachana na kama kuwa ya kufikirika. Tafiti zinasema unahitaji kiasi cha gharama kama $80,000 na ujuzi mkubwa katika masuala ya Engineering

2. kama sio Robert Downey Jr basi tungemuona Tom cruise ambae kampuni kwa kiasi kikubwa ilitaka nae kucheza role ya Tony Stark

1. Ni tajiri mkubwa sana ambapo anashikilia namba 36 katika list ya matajiri duniani lakini kumbuka hiyo ni ki filamu filamu tu na si ki maisha halisi.

No comments:

Post a Comment

Pages