Tomb Raider 2 Inakuja Kinamna Hii,Yupo Mkali Wa Into The Badlands Sunny - teknomovies
Tomb Raider 2 Inakuja Kinamna Hii,Yupo Mkali Wa Into The Badlands Sunny

Tomb Raider 2 Inakuja Kinamna Hii,Yupo Mkali Wa Into The Badlands Sunny

Share This
Filamu ya kwanza ilitoka mwaka 2001 huku ikiwa imesimamiwa vyema na Angelina Jolie ambae alisifiwa sana kwa uwezo wake aliouonesha ila filamu ilipondwa hasa katika mtiririko wa Action zake na hasa muundo wake japo ilifanya vizuri sokoni.

Safari hii inarudi tena lakini Si Angelina Jolie tena bali kazi hii kapewa mwigizaji ambae anakuja kwa kasI Alicia vikander.

Katika mchongo huo mpya pia tutaona sura ya Daniel Wu “Sunny” kama wengi ambavyo wamemjulia katika Into the Badlands.

Daniel Wu
Pia mtaalamu mwinginwe Nick Frost pia ataonekana vyema, wengi humwita Kibonge mwepesi ambae nae atakinukisha Ndani.

Nick Frost
Swali kubwa ni Je Alicia Vikander ataweza kuifanya kazi kama ilivyofanywa na Angelina Jolie.
March 16 mwaka 2018 kila kitu kitafahamika rasmi na tutaweza kutoa Credit zetu lakini kwa Trela linavyoonekana inaonesha itaweza kuwa kali japo Trela si kipimo sahihi.

Tazama hapo chini Trailer na pia Usisahau kutufuata katika mitandao ya Instagram na Twitter @Teknomovies
            

No comments:

Post a Comment

Pages