Young Dee Na Dogo Janja Wamekiwasha Sasa. - teknomovies
Young Dee Na Dogo Janja Wamekiwasha Sasa.

Young Dee Na Dogo Janja Wamekiwasha Sasa.

Share This
BAADA ya Young Dee kusema kuwa yeye sio wa kufananishwa na Dogo Janja na Young Killer na kutaka Waandishi wote wasimfananishe na Wasanii hao,Dogo Janja amekuja juu kwa kujibu kauli hiyo huku akisema hawezi kubishana na mtu anaetumia unga.

Akiongea na Teknomovies, Dogo Janja anasema hawezi kumjibu msanii huyo kwani hajui pia kama atakuwa anamjibu mtu mwenye akili timamu au tayari amekula unga.

Akaongeza kuwa Young Dee kuomba asifananishwe na msanii kama yeye ni sawa kwani hata yeye hataweza kukubali kufananishwa au kukaa na mtu anaetumia dawa za kulevya kitu kinachomfanya awe anazungumza vitu vya ajabu.

"Young Dee ni Mteja, na hawezi kufanana na mimi. Mtu mwenye akili timamu hawezi kutukana kwenye media matusi makubwa kama alivyofanya Young Dee. Akiacha Unga ndio ninaweza kuzungumza kitu kuhusu yeye, kwa sasa hivi nikimzungumzia siwezi jua kama ntakua nabishana na yeye au mteja. Mtu mwenye akili timamu unamsamehe tu maana inawezekana kashavuta mambo yake na yupo kwenye dunia yake nyingine" 


"Mimi pia sipendi kufananishwa japo sijakataa kufananishwa, Young Killer mimi nilishawahi kuwa role model wake kwa hiyo kufananishwa naye si kitu kibaya lakini kunifananisha na mla unga ni kukosea. Young Dee akiacha kula unga tutakaa mezani kuzungumza lakini kufananishwa naye sasa hivi sitaki kwani ni mtu ambaye ukimuacha gheto unawaza kama utaikuta TV " alisisitiza zaidi.

Young Dee alipoulizwa juu ya kauli ya Dogo Janja, anasema kwa kauli anazoongea Dogo Janja anamkosea sana heshima sababu kwanza yeye ana mchango mkubwa sana kwenye muziki wake na kuongeza kuwa ikibidi atamfundisha adabu.

"Yeye kama anaongea kuhusu suala la madawa inabidi awe na ushahidi, kwa sababu mimi nimeongea niko na ushahidi kwamba kimuziki asingekuwepo Young Dee wala wao wasingekuwepo, mimi nina mchango kwenye muziki wao, aliposikia mimi naongea vile ilibidi ajiulize kwa nini nimekasirika, sasa kuanza kurusha maneno inaonyesha ni upumbavu na hana akili, inaonyesha ni jinsi gani bado mtoto,”


"Unajua unakuwa mstaarabu sana lakini kuna muda unashindwa, mimi sijawahi kumuimba mtu, lakini hawa machalii wamekuwa wakiniimba kila siku sasa inabidi ifike mwisho,” aliongeza zaidi.

No comments:

Post a Comment

Pages