Aslay Ataja Sababu Ya Kuachia Nyimbo Nyingi Kwa Muda Mchache. - teknomovies
Aslay Ataja Sababu Ya Kuachia Nyimbo Nyingi Kwa Muda Mchache.

Aslay Ataja Sababu Ya Kuachia Nyimbo Nyingi Kwa Muda Mchache.

Share This
MSANII anaekimbiza kwa ngoma nyingi kwa sasa amefunguka juu ya sababu ya kuachia ngoma nyingi kwa kipindi kifupi kuwa ni kutokana na Yamoto Band ambapo nguvu nyingi zilikuwa huko.

“Kwa sasa naachia kazi nyingi kutokana na kwamba kipindi tukiwa Yamoto tulikuwa tunafanya sana kazi za kundi lakini kwa sasa kila mmoja anaweza kufanya kazi kivyake imenibidi niachie ngoma nyingi ili hata nikienda kufanya shoo niwe na nyimbo nyingi za kwangu,”

“Hivyo nitaendelea kuachia ngoma kali zaidi mpaka nitapoona hapa inafaa kusimama kwa muda basi nitasimama kwa muda ila watu waendelee kutegemea kazi kali zaidi,” aliongeza.


Mpaka sasa Aslay ameweza kuachia kazi zaidi ya sita ambazo zinaendelea kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya habari na kuendelea kukimbiza kwa watazamaji katika mtandao wa Youtube.

No comments:

Post a Comment

Pages