MIJI 5 HATARI ZAIDI HAPA ULIMWENGUNI. - teknomovies
MIJI 5 HATARI ZAIDI HAPA ULIMWENGUNI.

MIJI 5 HATARI ZAIDI HAPA ULIMWENGUNI.

Share This
Hatari ipo karibu nasi wakati wote, ajali pia tunatembea nazo ingawa hatujui muda na wakati gani hutokea ,  watu wengi wameuawa bila kutarajia kwa kupigwa risasi, mafuriko, na hata kuzama! Kisha kuna hatari za ndani, kama kasoro za moyo ambazo zinaweza kuua mtu mara moja, au ubongo kupata hitilafu. 

Ni ukweli kabisa hakuna njia maalum  ili kuepuka baadhi ya hatari katika maisha yetu ya kila siku, lakini tunaweza kufanya hatari hizo zipungue kutokana na mienendo yetu. Hii hapa ni list ya miji mitano hatari zaidi duniani.

5. Kabul, Afghanistan
Afghanistan ni nchi yenye vita, wakati wote majeshi ya magharibi yamepiga kambi hapo kusambaratisha vikosi vya kigaidi kama Al-Shabaab. Kujiua kwa mabomu (Kujitoa mhanga) ni kawaida sana kusikia kwani ni kama desturi.
Hili ni eneo hatari zaidi katika mataifa ya Asia.

Kabul Afghanistan
4. Cape Town, South Africa

Hili nalo ni moja ya eneo hatario zaidi duniani ingawa kwa kiasi kikubwa idadi ya vitendo vya kihalifu imepungua, sababu kuu inayofanya eneo hili kuwa na hatari zaidi ni kutokana na kuwepo kwa idadi ya wahamiaji wanaoingia mjini humo. Usishangae kufika Cape Town na kukuta  dawa za kulevya zikiuzwa kama njugu kwani ndio tabia ya mji huo na inakadiriwa ni zaidi ya 14% ya vijana huongezeka kila mwaka katika matumizi ya dawa za kulevya.

Vipo vikundi vinavyojihusisha na uhalifu wa kuvunja milango na kuingia majumbani kisha kupora na muda mwingine huua kabisa.


3. Caracas, Venezuela
Kifo cha Rais Hugo Chavez mwaka 2013 imeonekana kama ni matokeo ya kuongezeka kwa uasi katika mji mkuu wa nchi hiyo. 
Wananchi mara nyingi wanaingia mtaani kuandamana na kushinikiza serikali iliyopo idhibiti masuala ya rushwa pia huripotiwa vifo vya mara kwwa mara. Vikundi vya kihalifu huongezeka siku hadi siku hali inayopelekea ukosefu wa amani katika nchi hiyo. 

2. San Pedro Sula, Honduras
Hakuna shaka kwamba Honduras inapokea wageni wengi wa kitalii kutokana na hali yake ya kuvutia ya kitropiki. Uhalifu unafanyika sana katika maeneo ya San Pedro Sula, na watalii mara nyingi ni waathirika wa utekaji nyara na uhalifu mwingine wa kifedha na mara nyingi wanauawa. San Pedro Sula ina bahati mbaya ya kuwa mji mkuu unaoongoza kwa mauaji dunia nzima.
1   1.  Aleppo, Syria
Dunia nzima inafahamu hali ya kisiasa nchini Syria, mapigano ya kijeshi ni ya kawaida. Wakazi wengi wa Aleppo wanaishi kwa hofu kama wakimbizi na wamekimbilia juu ya mpaka katika nchi jirani ya Uturuki. Maisha ya mapigano ni maisha ya kila siku na ni  magumu zaidi kutokana na ukosefu wa mahitaji ya msingi kama vile umeme na maji ambavyo mara kwa mara huvurugika au kukatwa kabisa.


 Usisahau kuacha comment yako na kutufollow Instagram na Twitter @TeknoMovies

No comments:

Post a Comment

Pages