Msitu wa Saihanba wenye ukubwa wa hekta elfu 74.7
ulioko kilomita 200 kaskazini mwa mji wa Beijing nchini China, ni msitu mkubwa
zaidi duniani uliopandwa na watu. Wafanyakazi wa shamba la msitu huo wametimiza
muujiza wa kubadilisha jangwa kuwa msitu katika zaidi ya nusu karne iliyopita.
Kila ifikapo majira ya joto, msitu wa Saihanba unakuwa na mandhari ya
kupendeza. Upepo unavuma kwenye misonobari, mimea mingi inakua kando ya mito,
wadudu na ndege wanatoa milio, mambo yote hayo yamewavutia watalii wengi.
Taasisi ya misitu ya China imekadiriwa kuwa, msitu wa Saihanba si kama tu
unasaidia kuhifadhi rasilimali ya maji na kusafisha maji, bali pia inaweza
kutoa hewa ya Oxygen inayokidhi mahitaji ya watu milioni 2 katika mwaka mmoja.
Wakati watalii wanapohisi upepo wa fufutende unaopita msitu wa
misonobari, ni vigumu kwao kujua jinsi msitu huo ulivyopandwa katika miaka
mingi iliyopita. Mfanyakazi mstaafu wa shamba la msitu huo Bw. Zhang Baozhu
anasema
Mwaka 1962, serikali ya China ilianzisha shamba la msitu wa Saihanba.
Wafanyakazi 369 ambao wastani wa umri wao ni chini ya miaka 24 walikwenda
kwenye shamba hilo lenye mazingira magumu ambayo theluji inakuwepo kwa miezi 7
kila mwaka, na joto linaweza kufikia nyuzi 43 chini ya sifuri katika majira ya
baridi. Jambo linalowasikitisha zaidi ni kwamba katika miaka miwili ya mwanzo,
chini ya asilimia 8 ya miti walioyopanda ilistawi.
Kaskazini mwa msitu wa Saihanba wenye urefu wa mita 1500 kutoka usawa wa
bahari, ni jangwa la Hunshandake ambalo ni moja kati ya majangwa kumi makubwa
nchini China, na kusini nwa msitu huo ni miji ya Beijing na Tianjin.
Zamani upepo wenye mchanga uliingia Beijing kupitia eneo hilo, lakini
sasa msitu huo umezuia vizuri mchanga wa jangwani kupeperushwa kusini. Takwimu
zinaonesha kuwa siku zenye mchanga na vumbi angani katika majira ya mchipuko
mjini Beijing zimepungua kwa asilimia 70 kuliko miaka 50 karne iliyopita. Hali
ya hewa na mazingira ya msitu wa Saihanba pia imeboreshwa, sasa aina 1,757 za
wanyama na mimea inaishi katika msitu huo.
Wafanyakazi wa shamba la msitu wa Saihanba wanaanza kufikiria matumizi
endelevu ya rasilimali za msitu huo. Naibu mkuu wa shamba hili Bw. Chen Zhiqing
anasema,
Wafanyakazi
wamejitahidi kuendeleza shughuli za kukuza miti midogo, utalii na uzalishaji wa
umeme kwa nguvu ya upepo, na pia wamejionea mabadiliko kwenye maisha yao.
Wafanyakazi wengi wamepata nyumba mpya katika kaunti ya Weichang iliyoko karibu
zaidi na msitu huo, na wengi wamenunua magari.
Hayo ndio wenzetu wameweza kufanya na kuushangaza ulimwengu kwa kufanya Jangwa kuwa msitu mkubwa ambao ndege nao hutumia kama makazi....Watu wakisema hakuna kinachoshindikana chini ya jua ujue wanamaanisha.
Tufuate Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Update mbalimbali lakini pia usisahau kudownload Teknomovies App ili uwe wa kwanza kupata mastori makali.
Interesting
ReplyDelete