Simu ni kifaa cha mtu binafsi, lakini kuna baadhi ya watu hupenda kuchungulia meseji za wenzao hasa wanapoandika wakiwa kwenye eneo la watu wengi.
Tabia hii humkosesha mtu uhuru wa kuandika ama kusoma meseji katika eneno la watu wengi . Sasa kuliona hili watafiti kutoka kampuni ya Google wanafanya utafiti wa kuzuia mtu asiweze kuchungulia meseji zako.
Watafiti hao wanafanya majaribio ya sehemu ambayo pale unapokuwa unaandika au kusoma meseji kama kuna mtu anachungulia meseji nyuma yako basi hapo hapo kamera ya mbele ya simu yako itawaka na kumuonyesha pamoja na ujumbe kutokea kuwa kuna mtu anasoma meseji yako.
Kwa kutumia mfumo wa Facial Recognition wataalamu hao kutoka Google wameweza kufanikisha hilo huku teknolojia ikitegemea kamera ya mbele ili iweze kufanya kazi.
Kwa sasa watafiti hao bado wanaendelea na majaribio ya kujua namna gani itatumika kwa ufanisi zaidi kwani itakubidi uwashe kamera yako muda wote kitendo ambacho kinaweza kumaliza Chaji kwa haraka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mhariri Pia Mwandishi Mkuu Katika Tovuti Hii, Usiache Kupitia Kila Siku Kwa Habari Moto Moto.
No comments:
Post a Comment