Wema Sepetu:"Nauchukia Umaarufu,Sababu Nashindwa Kufanya Mambo Mengine Kama Binadamu" - teknomovies
Wema Sepetu:"Nauchukia Umaarufu,Sababu Nashindwa Kufanya Mambo Mengine Kama Binadamu"

Wema Sepetu:"Nauchukia Umaarufu,Sababu Nashindwa Kufanya Mambo Mengine Kama Binadamu"

Share This
Mrembo na pia Mwigizaji Wema Sepetu amefunguka kuwa kuna muda ambao anajutia sana umaarufu alionao kwa sababu kuna mambo mengine anatamani kufanya kama binadamu lakini anashindwa.

Akiwa na takribani miaka 11 hajawahi kupanda daladala tangu alivyoshinda taji la Miss Tanzania mwaka 2006,Wema anasema anatamani kwa namna anavyowaona watu mbalimbali wakiwa kwenye daladala wakiwa wanafurahi huku yeye muda mwingi akitumia gari lake.


Unajua kiukweli kabisa natamani mno kupanda daladala, kw a sababu hata mimi ni binadamu, kuna kipindi natamani kupanda gari kutoka kwangu mpaka Kariakoo au mpaka Mbagala, lakini unafikiria utakapopanda itakuwa ni vurugu na siyo starehe tena, huu umaarufu kwa kweli unani-’cost’ sana wakati mwingine,” alisema Wema. 

Pages