EXCLUSIVE : FORBES YATOA ORODHA YA MATAJIRI MAREKANI, TRUMP AANGUKIA PUA - teknomovies
EXCLUSIVE : FORBES YATOA ORODHA YA MATAJIRI MAREKANI, TRUMP AANGUKIA PUA

EXCLUSIVE : FORBES YATOA ORODHA YA MATAJIRI MAREKANI, TRUMP AANGUKIA PUA

Share This
Jarida maarufu duniani la FORBES limechapisha orodha ya matajiri wakubwa katika taifa la Marekani, Orodha hiyo imejumuisha idadi ya matajiri 400 huku rais wa Taifa hilo Donald Trump akiangukia pua kwa kupoteza kiasi cha $ 600 million kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Rekodi iliyowekwa kwenye orodha hiyo ni kwamba utajiri umekuwa kutoka $ 1.7 billion hadi $ 2 billion, na ukijumlisha mali wanazomiliki matajiri wote zinafikia kiasi cha $ 2.7 Trillion kutoka $ 2.4 Trillion kwa mwaka jana.

Katika Orodha hiyo jumla ya matajiri 22 ni wapya huku wengi kati yao ni wajasiriamali na waliopo 10 bora kila mmojawapo ametengeneza angalau $ 1 Billion kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Kwa mara ya 24 mfululizo namba moja imeshikiliwa na mmiliki wa Microsoft Bill Gates ambae anakadiriwa kuwa na utajiri wa $ 89 billion ambao utajiri wake umekuwa kwa $ 8 billion kwa kipindi cha mwaka mmoja. Namba mbili imeshikiliwa na Boss wa Amazon Jeff Bezos ambae utajiri wake umekuwa kwa kiasi cha $ 14 billion na kufikia kiasi cha $ 81.5 billion. Namba tatu imeshikiliwa na Warren Buffet ambae utajiri wake umeongezeka kwa kiasi cha $1.2 billion. Mark Zuckerberg mmiliki wa mtandao wa Facebook anashikilia nafasi ya nne huku akishika nafasi ya kwanza kwa mtu aliyeongeza kiasi kingi cha fedha kwa muda wa mwaka mmoja, ameongeza kiasi cha $ 15 Billion


Story kubwa kuliko zote inamuangukia rais wa Marekani ambae anahesabika kama mpotezaji mashuhuri (Most Notable loser). Kwa kipindi cha Mwaka mmoja Trump amepoteza jumla ya $ 600 million na kuwa na kiasi cha $ 3 Billion huku soko la hisa la Marekani likitetea kwa kutoa hoja kuwa huenda amepoteza kiasi hicho kikubwa kutokana na harakati za uchaguzi wa 45 wa taifa hilo.

Hii hapa Orodha ya matajiri 10 wa Marekani kwa Mwaka 2017.

1. Bill Gates                         $ 89 Billion

2. Jeff Bezos                        $ 85 Billion

3. Warren Buffett                $ 78 Billion

4. Mark Zuckerberg            $ 71 Billion

5. Larry Ellison                  $ 59 Billion

6. Charles Koch                 $ 48.5 Billion

7. David Koch                    $ 48.5 Billion

8. Michael Bloomberg       $ 46.8 Billion

9. Larry Page                      $ 44.6 Billion

10. Sergey Brin                   $ 43.4 Billion


Mwanamke wa kwanza amechomoza kwenye namba 13 ambae ni Alice Walton mwenye utajiri wa $ 38.2 Billion huku Donald Trump Akitupwa hadi nafasi ya 248 akiwa na utajiri wake huo wa $ 3 Billion.

Source : Forbes.com

Usisahau Kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Updates mbalimbali lakini pia Subscribe Youtube Channel ya DM Online Tv.

Pages