Mjue Angel Bernad,Mwanamuziki Mkali Wa Injili - teknomovies
Mjue Angel Bernad,Mwanamuziki Mkali Wa Injili

Mjue Angel Bernad,Mwanamuziki Mkali Wa Injili

Share This
Nani mpenzi wa nyimbo za injili ambae atakua haujui wimbo wa Siteketei

Kama unapenda kusikiliza nyimbo za injili hususani kutoka kwa wasanii wa Afrika mashariki basi Jina Anjela Bernard Lyamba Maarufu kama Angel Bernad Halitakua Geni kwako yote sababu ya ubora anaounesha katika masafa ya waimbaji wa nyimbo za injili.

Katika Familia yao, Angel anasema yeye ni mtoto wa Tatu, kati ya Watoto sita ,ambapo wavulana wapo watatu na wasichana pia watatu.

Na kwa upande wa Elimu kasoma shule ya msingi Kisutu, Na Sekondari Alisoma shule ya Zanaki na Mbezi Beach High School, O Level ikiwa Zanaki Na Advance ikiwa Mbezi High school akichukua masomo ya Sanaa.

SOMA PIA:HAMISA KAMUWASHIA MOTO IDRIS SULTAN

Na Chuo alimaliza katika chuo kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) akipata Digrii yake ya mambo ya Uongozi.

Kingine, labda watu wanaweza wakawa hawajui kuhusiana na hili, Angel anasema kua Alianza kuimba muziki wa Bongo Flavor kabla hajaingia katika mziki wa injili, Lakini kuanzia Mwaka 2009 ndipo alipoamua kuacha kabisa nakuamua kufanya muziki wa Injili Rasmi na kumtumikia Mungu.

Yeye mwenyewe anasema kua aina za nyimbo za injili anazoimba zinaitwa kwa sasa na watu wengi kama  Morden Gospel(Muziki wa injili wa Kisasa) ,yote ni kwasababu ya aina ya uimbaji wao uko tofauti sana na jinsi ilivyozoeleka lakini yote kwake anaona ni sawa tu.

Katika muziki wa injili anasema rasmi alianza kusikika pande mbalimbali na watu pale alipotoa albamu yake ya kwanza iliyotoka mwaka 2006 iliyokwenda kwa jina la Yote Yalikwisha.

Albamu yake ya Pili aliichia mwaka 2010,ambayo aliipa jina la Nakwabudu Milele Na albamu ya tatu aliichia mwaka 2014 akiipa jina la New Day.

SOMA PIA:TROLLS FILAMU BORA YA ANIMATION IPATE HAPA

Kuanzia mwaka 2014,ndio mwaka alioanza kufahamika sana sana kwa wengi na mpaka sasa Ameweza kujizolea mashabiki wengi hasa kutokana na uwezo wake wa kuinyumbulisha sauti yake kwa jinsi anavyotaka yeye.

Ukiachana na kazi yake ya Siteketei ambayo imepata umaarufu mkubwa, pia kuna nyimbo nyingine ambazo zinapatikana katika mtandao wa Youtube katika akaunti yake akitumia jina la Angel bernad kama baadhi....

Nikumbushe wema wako

Salama

Need You to Reign

Kiu yangu

Ni wewe

Have Your way na nyingine baadhi ambazo zimefanywa na video zenye ubora mkubwa sana na pindi utapotazama mojawapo ya hizo kazi, hakika utafurahi sana na kubarikiwa kama mimi nilivyobarikiwa kwa kutazama.

Changamoto kubwa anayokumbana nayo, anasema ni Hasa namna ya muziki wake wa injili anavyoimba baadhi ya watu wamekua waki kejeli kwamba ni mziki wa kidunia na haufai kuitwa mziki wa injili.

Pia Angel anaamini mziki wa Injili inatakiwa uchezwe sehemu yoyote ile, hata Katika kumbi za starehe sababu ndiko sehemu sahihi, kwani Mziki wa injili haufanywi kwaajili ya watu walio okoka Tu, bali inawahitaji hata wasio Okoka Kuweza kusikiliza nyimbo hizo.

Huyo ndo Angel Bernad ambaye anazidi kuifanya kazi ya mungu Kwa ustadi na weledi katika uimbaji.

Unaweza ukaacha maoni yako, Wimbo gani kutoka kwake ukiusikiliza hua Unabarikiwa Sana nazani akiona, atafarijika sana kuona kazi yake inapendwa.

Unaweza kutazama Videos Zake Mbalimbali Kwa Kubonyeza HAPA

Vyanzo: Ayo Tz na Mitandao Mingine.





Pages