WANAJESHI WAMTEMBEZEA KICHAPO DALALI WA MAGARI KISA? - teknomovies
WANAJESHI WAMTEMBEZEA KICHAPO DALALI WA MAGARI KISA?

WANAJESHI WAMTEMBEZEA KICHAPO DALALI WA MAGARI KISA?

Share This
Duniani hakuishi vituko, ni hivi karibuni tu wanajeshi mkoani Tanga walimpiga kondakta wa daladala hadi kumsababishia kifo. Sasa tukio jingine limetokea huko Nigeria eneo la Coma baada ya dalali kushindwa kumuuzia mteja wake (Ambae mwanajeshi) gari walilokubaliana.

Dalali huyo alikubaliana kila kitu na mteja wake kilichobaki ilikuwa ni malipo tu ambapo dalali alitaka Naira 500,000 ila wakati mteja wake yuko kwenye mchakato wa kulipa, akajitokeza mteja mwingine mwenye dau kubwa ndipo akamuuzia.

Baada ya kumuuzia punde mteja wake wa awali akajitokeza na kumkuta dalali huyo amekwishaliuzwa gari hilo.

Na maamuzi aliyoyachukua mteja huyo ni kwenda kuwaita wanajeshi wenzake 4 ili waje wamfundishe adabu dalali huyo.

No comments:

Post a Comment

Pages