JAMAA KAMKUTA RAFIKI YAKE AKICHEPUKA NA MKEWE JUU YA KITANDA, HIKI NDICHO ALICHOKIFANYA. - teknomovies
JAMAA KAMKUTA RAFIKI YAKE AKICHEPUKA NA MKEWE JUU YA KITANDA, HIKI NDICHO ALICHOKIFANYA.

JAMAA KAMKUTA RAFIKI YAKE AKICHEPUKA NA MKEWE JUU YA KITANDA, HIKI NDICHO ALICHOKIFANYA.

Share This
Jamaa mmoja nchini Kenya katika eneo la kisiii amefanya maamuzi ya aina yake baada ya kumfuma mkewe akiwa na rafiki yake juu ya kitanda wakifanya yao.

Mkazi huyo aliyetambulika kwa jina la Richard Omoke (40) aliamua kukata mkono wa kushoto wa rafiki yake Vicent Gwaro (37) ambae ndie aliyechepuka na mke wa rafiki yake.

Inaelezwa siku ya tukio mnamo tarehe 17 February, watu hao walikuwa msibani lakini ilipofika majira ya saa 7 usiku Bwana Vicent na Mke wa Richard wakaondoka msibani bila kuaga wenzao ndipo Richard akaamua kufuatilia ni wapi wameenda. Na akawakuta katika nyumba ya wageni iliyo karibu na eneo la msiba.

Bwana Richard akachukua Panga lililokuwepo kwenye chumba cha mlinzi na kumfuata rafiki yake Vicent kisha kukata mkono wake wa kushoto.

Baada ya tukio hilo Richard akachukua simu ya Vicent na kuwapigia watu walio kwenye msiba waende wakamchukue Vicent na walipofika walimkuta akilia kwa maumivu makali huku mkono ukiwa upo chini sakafuni.

Kamanda wa Polisi kutoka kituo cha Marani OCPD Benjamin Kimwele amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku juhudi za kumtafuta mtuhumiwa zikiendelea. Kamanda Kimwele amesema pia hiyo si mara ya kwanza kwa Vicent kuchepuka na mke wa mtu kwani mwaka 2016 aliwahi kushikiliwa kituo kwake kwa kosa kama hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages