Faida za kutumia Simu za Iphone
Programu Endeshi yake inafanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Moja ya jambo ambalo Apple wamewashinda Google basi ni katika mfumo wa Ios ambao unapatikana katika simu za Iphone,ni mfumo ambao unafanya kazi kwa ufanisi mkubwa na inampa mtumiaji uwezo mkubwa wa kuweza kufanya kazi kwa uhakika tofauti na mfumo wa Android ambao mara kadhaa umekuwa ukipatwa na kasoro.
Kupata Masasisho mapya (Updates)
Makampuni ya simu yanayotumia Android huwa yanachukua matoleo bora ya Android na kisha kuweka baadhi ya Apps inazohitaji na kufanya marekebisho na hiyo huathiri pindi Google wanapohitaji kufanya Updates kuchelewa lakini kwa upande wa Iphone pindi sasisho jipya linapotokea basi watumiaji wengi mara moja hupata huduma hiyo na hivyo kuwafanya wengi kufurahia
Muonekano bora wa utumiaji
SOMA PIA:MAKOSA AMBAYO YAMEFANYWA KATIKA BAADHI YA FILAMU
Kwa ambao hawapendi kuchezea sana simu,yani kutumia simu kwa ni kupiga na kupokea,Kupiga picha na kutuma meseji basi simu za Iphone ni rafiki sana katika hilo kwa sababu ina muonekano rahisi usio na kashi kashi yoyote.
Apps
Katika mfumo endeshi wa Iphone,Apps zake ni bora sana kwa sababu ya ufanisi ambao upo katika kuruhusu Apps kuwekwa hivyo ni kazi kupata App ambazo zinafanya kazi chini ya kiwango,Lakini kwa mfumo wa Android mara kwa mara imekuwa ikitokea uwepo wa Apps ambazo zipo chini ya kiwango ambazo pia muda mwingine huaribu utendaji kazi wa simu.
Hizo ni faida kadhaa vipi kuhusu Mapungufu ya simu za Iphone?
Utumiaji wa mafaili kutoka mitandaoni
Hapa kuna tatizo kidogo kwa watumiaji wa Iphone ambapo kushusha nyimbo kutoka mtandaoni huwa kazi badala yake mafaili kama pdf huwa ni rahisi kwa mtandaoni lakini kwa watu wa Android kwao huwa ni rahisi zaidi
Chaja
Ni ukweli halisi kuwa watumiaji wa Iphone ni wachache sana na pia muingiliano wa chaji kwa upande wa Iphone si rahisi tofauti na upande ya watumiaji wa Android ambao muingiliano wa chaja kwao ni simpo kwahiyo endapo mtumiaji wa Iphone ukisahau chaja yako basi itakuwa ni tatizo kwako kupata chaja.
Ugumu wa muonekano
Wakati kwa upande wa Android unaweza kubadirisha muonekano unavyotaka kwa kupakua baadhi ya themes,Kwa upande wa Iphone ni kazi kwa sababu inaruhusu kubadiri Wallpaper tu. Lakini kwa Android unaweza kubadiri muonekano katika sehemu nyingi na kuiweka simu na muonekano bora zaidi
Ishu ya Ujazo
Kama unataka ujazo mkubwa,basi wekeza pesa kubwa kununua Iphone ambayo itakuwa na ujazo mkubwa,lakini kwa upande wa Watumiaji wa simu za Android unaweza kununua simu yenye ujazo mdogo na ukaongezea na memori kadi kwa pesa kiasi kidogo na ukafurahia simu yako.
Ongezea mambo mengine ambayo unaona Tumesahau kuhusu Simu za Iphone.
Usisahau Kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Updates mbalimbali na pia Subscribe Youtube Channel ya DM Online Tv.
Source:teknokona.com
Ungana Nasi