App Ya Azam Tv Sasa Yaanza Kupatikana - teknomovies
App Ya Azam Tv Sasa Yaanza Kupatikana

App Ya Azam Tv Sasa Yaanza Kupatikana

Share This
App ya Azam TV. App ya kisasa kabisa ya AzamTV imeanza kupatikana rasmi katika Google Play Store na App Store ya Apple kuanzia Julai Mosi.

App hiyo iliyokuwa ipatikane tangu Juni mosi lakini ilishindikana, watu wataweza kutazama chaneli saba ambazo ni Azam ONE, Azam TWO, Sinema Zetu, ZBC 2, Azam Sports HD kwa Tanzania Pekee, na Real Madrid TV na NTV Uganda.

Taarifa moto moto za Kimichezo, Habari, Burudani na matukio mbalimbali yanayoendelea nchini na ulimwenguni pia yatapatikana kupitia App hiyo.

Kwa sasa Kuangalia chaneli hizo hakutatozwa pesa yoyote yaani ni bure ingawa mwanzoni ilitaarifiwa kulipia kwa Tsh 400 kwa siku, Tsh 2500 kwa wiki au Tsh 9000 kwa mwezi.

App ya Azam TV
Ili kuweza kufurahia huduma zao, hakikisha una bundle la kutosha tu na network nzuri ili uweze kufaidi vizuri huduma zao mahali ulipo na wakati wowote.

3G ndio mtandao wa chini kabisa unaotakiwa kuutumia kupata huduma hii kwenye AzamTV app.

Kituo kingine cha Runinga ambacho kilishatangaza App yao ni ITV ambayo inapatikana Google Play Store na App Store ya Apple

Source:Teknokona

Link ya Azam Tv Katika Playstore

Link Ya Azam Tv Katika App Store 

Pages