BREAKING NEWS: TYRESE AKIMBIZWA HOSPITALI KUFUATIA MAUMIVU MAKALI YA KIFUA - teknomovies
BREAKING NEWS: TYRESE AKIMBIZWA HOSPITALI KUFUATIA MAUMIVU MAKALI YA KIFUA

BREAKING NEWS: TYRESE AKIMBIZWA HOSPITALI KUFUATIA MAUMIVU MAKALI YA KIFUA

Share This
Star wa Fast and  Furious Tyrese Gibson (38) amepata maumivu makali kwenye kifua baada ya kutokea mgogoro kati yake na mzazi mwenzie Norman Gibson.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ ni kwamba baada ya kutokea mgogoro kati yake na mzazi mwenzie juu ya masuala ya kulea mtoto, Tyrese alirejea usiku wa october 26 hotelini alipokuwa amepanga na baada ya muda mfupi alianza kupata maumivu kwenye kifua.

Chanzo cha cha habari kinasema baada ya Tyrese kupatwa na maumivu hayo alikimbizwa Hospitalini kwa ajili ya vipimo na kujua chanzo cha maumivu hayo.

Norman amepeleka shtaka mahakamani kuwa Tyrese amemtelekeza mtoto wao mwenye umri wa miaka 10 kwa kutopeleka mahitaji kwa mtoto huyo kama yalivyoainishwa kwenye hati kuwa kila mzazi atoe 50% ya malezi kwa mtoto wao.
Siku moja kabla ya kupelekwa Hospitali Tyrese alipost picha Instagram akiwa na mkewe mpya Samantha Lee huku akiweka caption ya kusema "Safari ya mahakamani, mnahitaji kuujua ukweli na nani ni mshindi"

Usisahau Kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Updates mbalimbali na pia Subscribe youtube Channel DM Online.

Pages