Boss wa Hollywood alitaka kuhonga $1 million ili afichiwe siri - teknomovies
Boss wa Hollywood alitaka kuhonga $1 million ili afichiwe siri

Boss wa Hollywood alitaka kuhonga $1 million ili afichiwe siri

Share This
Mwigizaji wa kike Rose McGowan amefichua siri kuwa boss wa Hollywood Harvey Weinstein alitaka kumpa $ 1 million ili asitoe siri ya kuwa alimnyanyasa kingono miaka ya 90's.


Rose anamtuhumu Weistein kuwa alim'baka huku mastaa wengine kadhaa nao wametoa mashtaka juu ya boss huyo kuwa walinyanyaswa kijinsia. Katika mahojiano yake na jarida la The New York Times, Rose amesema boss huyo alitaka kumpa pesa hizo kipindi ambacho wanaandaa movie ya Mogul.

Rose ameongeza kuwa suala hilo hakuwahi kumwambia mtu kwani alihisi angekosa nafasi kwenye utayaerishaji wa movie mbalimbali ambazo zinasimamiwa na kampuni ya Weinstein.


Ni mwezi mmoja sasa tangu wasanii wa kike kutoka Hollywood walipoanzisha kampeni maalum kwenye mtandao wa twitter wa kufichua maovu wanayofanyiwa na maboss wa Hollywood ambapo kampeni hiyo imepewa Hashyag ya MeeToo (#MeToo) .

Swali la kizushi je kampeni hii inaweza kufanyika Afrika hususani Tanzania?

Usisahau kuacha Comment yako na Kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Updates mbalimbali na pia Subscribe Youtube channel ya DM Online Tv.

No comments:

Post a Comment

Pages