NIKOLA TESLA:: MWANASAYANSI NGULI KUWAHI KUTOKEA DUNIANI - teknomovies
NIKOLA TESLA:: MWANASAYANSI NGULI KUWAHI KUTOKEA DUNIANI

NIKOLA TESLA:: MWANASAYANSI NGULI KUWAHI KUTOKEA DUNIANI

Share This
Alizaliwa Ulaya Mashariki kwenye nchi ambayo leo ni Croatia/Serbia. Kipindi ambacho kulikuwa na option mbili tu Kujiunga na Jeshi au dini.

Baba yake alikuwa ni Mchungaji wa kanisa na mama yake alikuwa mama wa nyumbani. Alilazimishwa kujiunga na kanisa lakini alikataa hakuwa tayari. Mama yake kakuwahi kwenda shule lakini alikuwa na talent ya kushona na uwezo mkubwa wa kukariri mashahiri vitu vilivyomfanya mtoto Tesla kuvutiwa Sana.

Vitu hivi vilimfanya kuwa na uwezo wa kufanya hesabu ngumu za CALCULUS (watu wa Hisabati mnanielewa) kwa kichwa kitu kilichowafanya waalimu wahisi anadanganya au kunasehemu anaangalizia.

MAISHA YA AWALI

Akiwa mtoto mdogo aliposoma kuhusu maporomoko ya Niagara Marekani kichwani mwake aliona Gurudumu likizunguka katikati ya maji. Kwa immagination na meditation akajakuwa founder wa umeme wa maji miaka mingi baadae alipofika hilo eneo.

SOMA PIA: KIFO CHA BRUCE LEE

Kuna kipindi akiwa chuo alikuwa akisoma kuanzia saa tisa usiku hadi saa tano usiku mfululizo. Hadi siku moja akiwa nyumbani akakuta barua ya siri ya Proffesor akimuandikia baba yake wamrudishe nyumbani maana akiendelea atafariki.

KISA CHA KWENDA MAREKANI

Akiwa na upenzi wa sayansi alipata kazi katika viwanda. Baadae alienda Ujerumani alipopata kazi kisha akaajiriwa na kampuni ya kimarekani ya umeme DC General Electric ya Thomas Edison founder wa DC current. (Umeme wa DC hutolewa sana na Betri).

Waliokuwa na tawi Ufaransa. Kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha akapata transfer kwenda makao makuu ya kampuni hiyo Marekani afanye kazi ya kudesign na pia atakuwa karibu zaidi na Edison.
Akaingia New York akiwa bado kijana sana.

KUTOKA KUWA MTAALAMU HADI KUCHIMBA MITARO KAMA KIBARUA

Akifanya kazi bila kuchoka, akifanya design, siku moja bosi wake Edison alimuambia akidesign system ambayo itasaidia kuboresha ufanisi wa mashine zake atapewa dora 50 ambayo ilikuwa pesa nyingi kwa wakati huo. Alipofanikiwa jamaa akamgeuka akamwambia alikuwa anamtania. Jamaa akaamua kuacha kazi hata baada ya kulazimishwa saana. Alichokutana nacho ni maisha magumu kupita kiasi. Ilifika kipindi akawa anachimba mitaro, ili angalau apate pesa ya chakula. Hadi siku moja alipojiuliza kwa nini anafanya kazi za ajabu huku kichwani anaazina ya kutosha.

MVUMBUZI WA AJABU

Alikutana na jamaa ambao aliingia nao makubaliano ya wao watamsupport ktk vitu anavyokuwa akivumbua. Uvumbuzi wa DC motor alioufanya na baadae kuwa mshauri kwa kampuni pinzani ya Edison. Alijipatia pesa nyingi maana kwa uvumbuzi wake ulilingizia kampuni hilo mamilion ya pesa. Kitu ambacho kilihatarisha uhai wa kampuni yake aliyoacha kazi ya Mr Edison. Alikuwa halali zaidi ya masaa manne. Fedha hizo aliziingiza katika utafiti wake huku akiishi hotelini maisha yake yote hadi mauti inamkuta.

VITA VYA UMEME

Wivu wa uvumbuzi wa umeme mbadala wa edison ulimfanya jamaa kutumia fitna kuwatisha watu kua umeme huo ni hatari saana kwa uhai.

Edison alikusanya watu newyork akafanya maonyesho ya hatari. Kuua tembo, nyani kwa umeme wa AC. Watu walijaa hofu.

PITA HAPA PIA: MJUE MKALI WA IP-MAN NA BLOODMON

Tesla yeye aliwaita watu waje washuhudie jinsi alivyoweza kuzungusha yai bila kupasuka juu ya sahani kwa kutumia AC motor.

 Siku Edison aliponyamazishwa rasmi ni pale alipowanyima akina Tesla haki ya kutumia taa zake Za DC siku maalumu ambapo watu walitoka dunia nzima kuja kushuhudia uvumbuzi mwingine wa Tesla.

Tesla aliishangaza New York nzima, usiku ulipofika akiwasha taa zake mwenyewe kwa umeme wake ambao ulifunika jiji zima.

DC bulbs zikaonekana kama koroboi. Mji ukawa kama mchana.

MAAJABU YA KISAYANSI

Aliweza kutengeneza radi hata ndani ya chumba alichokuwa anafanyia utaafiti.
Alijenga mnara kwa mara ya kwanza alitaka umeme uwe wireless. Dunia nzima iwe na umeme bila hata waya.

Alipotengeneza wireless controlled boat waalikwa wa siku ya maonyesho waliona ni uchawi. Wakasema kuna nyani mdogo kamtrain ndio anaendesha baadae wakafungua hawakukuta kitu.

Akasema awauzie jeshi la marekani hiyo technology wakamdharau lkn leo mabomu,drones na vitu karibu vyote wireless huwezi kumsahau Tesla.

Mnara wa kwanza wa mawasiliano ulijengwa na huyu jamaa japo kwa lengo la kutransmit power alifanikiwa kupokea signal kwa mara ya kwanza zikitokea ulaya. Huku yeye na wenzake walidhani zimetoka mbinguni au sayari tofauti.

ANATUFUNDISHA NINI KATIKA KUKATA TAMAA

Akiwa katikati ya Uvumbuzi na utafiti wa X-RAY(ambayo baadae wakati akiwa na hili tatizo jamaa mwingine akavumbua) katika maabara yake, Hakuamini macho yake kesho yake asubuhi alipokuta maabara yake imeungua na kila kitu kimekuwa ni majivu tu. tesla alipoteza Mamia ya ,
1. Documents za mipango yake,
2. Design zake zote alizokuwa ameziandaa,
3. Notes , invention models
4. Picha zake alizokuwa amejitunzia pamoja na vitu ambayo alikuwa ameviandaa tayari kwa maonyesho.

Alipoteza kiila kitu, vitu vyote vilikuwa na thamani zaidi ya $50,000 miaka hiyo, alipoulizwa na gazeti ya New York times kuhusu janga lililompata, kwa huzuni na uchungu alisema, "I am in too much grief to talk, What can I say?", lakini alijikongoja akaanza upya kwa kuwa supported na sponsors waliomuamini na akafanya mambo makubwa zaidi ikiwepo wireless radio wave driven boat.

KUFA MASKINI HUKU AKIACHA WATU KUA MABILIONEA

Pamoja na mambo makubwa aliyofanya nikola tesla alikufa akiwa hana kitu. Alifia hotelini alipokuwa akiishi. Kazi kubwa aliyoifanya iliishia kuwafanya kuwa mabilionnaire. Mfano mwanasayansi wa italia Marconi ilipata tenda na patent kutoa huduma ya fax marekani baada ya kumshinda kesi Tesla. Lakini kiukweli karibu kila alichotumia ni ideas za Tesla na mfadhili wake Morgan akaamua kumuacha na kumsupport Marconi. Vitu karibu vyote alivyovumbua viliishia mikononi mwa wanasayansi makanjanja na kujitajirisha. Tatizo lake hakujielekeza kwenye haki miliki na pia yawezekana wamarekani hawakutaka kumpa umaarufu japo alichukua uraia. Kama angekuwa umiliki wa uvumbuzi wake leo. Angekuwa tajiri namba moja duniani maana krb kila kitu cha sasa anamkono wake.

AMEKUFA LAKINI KAACHA ALAMA ZA KUDUMU DUNIANI IKIWA NI MATUNDA YA MATUMIZI SAHIHI YA UBONGO WAKE.

Miaka ya sitini Tesla ilipitishwa kuwa SI unit ya Magnetic flux density (wale wa Physics Advance wananielewa) kumuenzi. Amekuwa kivutio kwa wanasayansi vijana enzi hizo akiwapo Albert Einstein ambaye anamuona kama role model. Baada ya kufa inasemekana makachelo wa marekani waliofika hotelini hapo waliondoka na mavumbuzi mengi yake ya kijeshi ndio maana wako vizuri kivita baada ya kudevelop.

Mfano wanasayansi leo wanafanya utafiti wa kusambaza umeme dunia nzima kupitia anga linaloitwa Ionosphere. Marekani wanafanya research ya kutumia reflecting satelite kupeleka umeme Japan. Zote hizo ni kazi za tesla zilizomfanya akaitwa Mwanasayansi KICHAA.

Baadhi ya vitu vilichukuliwa na ndugu zake zikapelekwa serbia na yawezekana wanasayansi wa urusi walitumia pia kudevelop vitu na silaa. Mitaa, vyuo, mabarabara, vikundi vya wasomi, taasisi za kisayansi vimeitwa kwa jina lake kumuenzi Great thinker huyu katika mambo ya science na technolojia

Pages