Polisi Wapekua Nyumba Ya Mbowe - teknomovies
Polisi Wapekua Nyumba Ya Mbowe

Polisi Wapekua Nyumba Ya Mbowe

Share This
Jana majira  ya jioni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alikamatwa na Polisi akiwa barabarani katika Daraja la Mlalakuwa lililopo Mikocheni na kufikishwa kituo cha polisi.Mbowe alikamatwa baada ya kupewa saa 48 kuanzia Jumamosi ambapo Kamishna Sirro alimtaka kiongozi huyo kujisalimisha kwa ajili ya mahojiano kufuatiwa kutajwa katika orodha ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.
Mbowe ambaye alikamatwa jana akitoka nyumbani kwake alikuwa ameambatana na dereva wake na walinzi wake alitoka kwenye gari lake na kuingia kwenye gari la polisi ndipo safari ya kwenda kituo cha polisi ikaanza.Hadi majira ya saa tatu usiku polisi walikuwa bado wakipekuwa nyumba ya Freeman Mbowe ili kuona kama kunakitu chochote kinachoashiria uwepo wa dawaza kulevya.Aidha, baada ya kupekuwa katika nyumba yake, Polisi walikwenda kupekuwa katika nyumba ya mkewe lakini hawakueleza kama walikamatadawa za kulevya katika maeneo hayo waliyopekuwa.Wakati huo huo haya yote yakiendelea, kesi ya Kikatiba aliyofungua Freeman Mbowe dhidi ya RC Makonda, Kamishna Sirro na Mkuu wa Uplelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam inatarajiwa kuanza kuunguruma katika Mahakama Kuu Dar es Salaam.Mbowe alifungua kesi ya kikatiba baada ya kutajwa na RC Makonda kwenye orodha ya watuhumiwa wanaojihusisha na biashara ya dawa z akulevya na kumtaka afike kituo cha polisi kwa ajili ya mahojiano.

No comments:

Post a Comment

Pages