KIJANA APATA ZAWADI YA KUSIKIA BAADA YA KUISHI BILA MASIKIO KWA MIAKA 15. - teknomovies
KIJANA APATA ZAWADI YA KUSIKIA BAADA YA KUISHI BILA MASIKIO KWA MIAKA 15.

KIJANA APATA ZAWADI YA KUSIKIA BAADA YA KUISHI BILA MASIKIO KWA MIAKA 15.

Share This
Kijana apata zawadi ya kisikia baada ya kuishi bila masikio kwa miaka 15
Madaktari wa upasuaji kutoka Cape town Afrika kusini, wamefanikiwa kuunganisha masikio kwenye kichwa cha kijana aliyezaliwa bila masikio.

Kijana huyo alizaliwa bila masikio wala mifereji ya masikio (ears canal) pia hakuwa nayo na ameishi katika hali hiyo tangu kuzaliwa kwake miaka 15 iliyopita.

Kwa umakini wa hali ya juu madaktari wameweza kuunganisha masikio bandia yenye uwezo wa kupokea mawimbi ya sauti na kumpa kijana huyo matumaini mapya katika maisha.

Anakuwa mtu wa kwanza kupokea upasuaji wa aina hiyo kwenye masikio ya binadamu katika hospitali ya Groote Schuur nchini Afrika kusini.

Kijana huyo mwenye miaka 15  Tylor baker alizaliwa bila masikio na mifereji ya sikio hali iliyomfanya ashindwe kusikia kwa muda wote.

No comments:

Post a Comment

Pages