MTOTO WA PELE MATATANI KWA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA. - teknomovies
MTOTO WA PELE MATATANI KWA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA.

MTOTO WA PELE MATATANI KWA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA.

Share This
Mahakama nchini Brazil imesema kwamba mtoto wa mwanasoka wa zamani nchini humo Pele, ambaye alikutwa na hatia ya kutakatisha fedha na biashara ya madawa, atatumikia kifungo cha miaka 12 na miezi 10 gerezani.

Edinho, ambaye jina kamili ni Edson Cholbi do Nascimento awali ilikuwa atumikie kifungo cha miaka 33 kuanzia 2014 lakini kutokana na kukata rufaa, mahakama imeridhia kumpunguzia adhabu. Edi(46) alishindwa kutumikia adhabu yake kwa kipindi chote hicho kutokana na rufaa yake kutosikilizwa kupisha chaguzi mbali mbali za mahakama na hukumu yake kutolewa rasmi Ijumaa 24. 2.2017

Hakimu ambaye amesimamia kesi hiyo ameridhia kupunguza adhabu hadi kufikia miaka 12 na miezi 10.

Licha ya baba yake mpaka sasa kutotoa maoni juu ya hukumu hiyo, Edinho ambaye alikuwa kipa kwa vilabu kadhaa nchini Brazil katika miaka ya 1990, ikiwa ni pamoja na klabu ya nyumbani ya  Pele FC Santos ametoa rai ya kuwa hati yake na kiapo cha kuendelea kupambana mashtaka iimarishwe.

Kwa upande wa Edi nae alisema
" Kiukweli nimechanganyikiwa sana kwa sababu mimi kutuhumiwa na fedha haramu na mimi kamwe sikuwahi kujihusisha, hakuna wa kwamba mimi najihusisha " aliwaambia waandishi wa habari.

No comments:

Post a Comment

Pages