Waraka wa Kwanza Heri Muziki Ameanza Kwa Kuandika.
"DIVA.
Muda uliopita nilikutana na msichana ambae sitamsahau kwenye maisha yangu, sitamsahau kwa mengi. Sitamsahau kwa namna alivyoniangalia na uzuri wa macho yake kila aliponitazama,sitamsahau kwa namna hisia zake zilinifanya nijiskie maana halisi ya upendo, sitamsahau kwa namna ambayo alijaribu kunijenga pia. Nakumbuka sana wakati mahusiano haya yalianza, nilikua nikishangaa kwanini mimi? Nikajihisi pia hivi kweli yule dada mzuri,mpendwa na wengi ana uwezo wa kunipenda mtu kama mimi? I still remember how that felt like and I will never forget.
Mahusiano yangu na huyu dada yalikua ni ya tofauti,furaha zilikuepo, na kupoteza pia kulikuepo ila upo muda kupoteza kulizidi kuliko kufurahi. Kama matani tu, wakati naanza na diva nilipoteza marafiki, kama matani tu watu walioniamini walianza kuhisi nimeanza kuishi maisha yangu kwa namna ya kupelekeshwa, kama matani tu maisha yangu yalibadilika kutoka kwenye kijana wa kawaida anaeimba na kuhangaikia na masomo shuleni mpaka kijana anaepoteza muelekeo kwa sababu zisizoeleweka.
Kama matani tu, hata baadhi ya familia yangu walihama upande wa kunitafakari,kuniona na kuhamia kwenye kuamini kila mwenzangu huyu anachokifanya, inshort ndani ya muda mfupi tu,uwepo wangu ulipoteza relevance, ndani ya muda mfupi tu kati yangu na wengine wote kulikua na ukuta,ukuta huu uliitwa diva,ilibidi wapite kwake kunifikia.
Kama matani tu,nilimpoteza heri ninaemfahamu,na kukutana na heri asiejipenda wala kupenda maisha yake yanapoelekea,Heri asie na amani. Na kama utani tu,mwanafunzi alieanguka ghafla ANGUKO kubwa sana chuo, kama utani tu, kiben10 mbele ya macho ya watu mwenye shida ya mafanikio ya diva tu.
Nakumbuka kuketi chini nikiwa na mawazo sana,hii siku chozi lilinitoka nikiwaza, hivi, yule heri mwenye ndoto za kuisaidia jamii, mwenye ndoto ya kukonga jukwaa, Mwenye mapenzi ya kweli, Mwenye familia nzima nyuma yake inayomfanya ahangaike na kutumia mpaka jasho lake la mwisho ili ainyanyue na yeye awe MTU siku moja, ndio huyu huyu ambae ninamuona hapa sasa? Amani yangu ya moyo ilipotea sana sana sana, na nilikua na uhakika kwamba sasa sihitaji mapenzi, nahitaji kujitafuta,namuhitaji heri ninaemjua,namuhitaji heri mpambanaji. INAENDELEA,"
Waraka Wa Pili
"Kwa mujibu wa maisha yangu na watu wanaonitegemea,sina muda kabisa na sitakiwi kuwa na muda hasa wa kujipoteza tena (loose myself).
Hapo ndipo niliposonga kwa diva, Takriban miezi mitatu iliyopita na kumueleza kwamba sitaweza kuwa na yeye tena, na sababu ni kwamba nataka kujitafuta mimi zaidi na pia kwangu yale hayakua mapenzi tena, alikiri kunielewa na ndipo nilipoanza safari yangu ya kujitafuta tena. Ndani ya miezi mitatu mimi na Diva hatuna mahusiano tena, ila hili lilionekana kuwa swala gumu sana yeye kulikubali, bado alijaribu kunifanyia favor nyingi ambazo upo muda nilimsisitiza sihitaji, na nahitaji maisha ya kujihangaikia mwenyewe ila haikuwa rahisi kufahamu. Kichwani kwake sasa nahisi, alikua in denial (kwenye kukataa) kwamba yule kijana aliempelekesha,aliemfanya mpaka aanguke kwenye masomo,kijana aliekua akienjoy kumuonea leo hayupo tena na nahisi hili ndilo lililotufikisha hapa leo.
Baada ya muda Diva alinitafuta na kuniambia ana project ambayo anaomba niishiriki,amenichagua mimi. Sababu nataka kupambana kujikomboa kimaisha nilikubali na kuanza kuifanya na hatimae kutoa wimbo wangu wa sasa wa #Waambie, nadhani mkiwa na kumbukumbu pia,hata yeye diva siku chache zilizopita alipost post ambayo alinitambua mimi kama #MdogoWake na kunishukuru kwa kushiriki kwenye project yake. Nahisi hii ilikua tosha kuonesha mahusiano na Diva hayajaisha wala kukanwa jana kwenye leo tena, bali #Hayapo. INAENDELEA,"
Waraka Wa Tatu
"Kiukweli na mapungufu yake yote Diva, siku zote nitamshukuru kwa muda wake aliotumia kuuwaza muziki wangu, kati ya wanawake ninaowaheshimu kwenye maisha yangu ni yeye. Na siwezi,wala #sitawahikuweza kumuadhirisha hata siku moja kwenye maisha yangu. Wakati Diva ananiita kwa ajili ya project nilihakikisha mimi na yeye tunafanya mazungumzo, na tuliamua pamoja kwamba kwa sasa mimi na yeye tunafanya kazi tu,alikubaliana na uamuzi huo na alisema yupo sawa tukiutamka pia.
Jana nilikwenda kwenye mazungumzo na leo tena nikijua nitazungumzia wimbo wangu mpya wa waambie, katikati nikashtukia tayari mazungumzo yamekwenda kwenye ndoa na diva,kitu ambacho hakipo na mimi na yeye hatupo pamoja. Ilinifanya nijihisi nahitaji kuweka clear kama makubaliano yangu na diva. Nanukuu kusema "Mimi na Diva tumeweka mahusiano pembeni,sasa tunafanya kazi". Ila kauli hii imechukuliwa kama kumkana na kumdhalilisha mtu ambae hata tulishakubaliana nae kwamba hiki ndicho tulichonacho.Ninaomba msamaha sana kwa wote niliowakwaza, Diva mama,unanifahamu vizuri sana kujua siwezi kukusudia kukudhalilisha hata siku moja, kama nilikosea jana,niamini sikukusudia, nilikua tu nasimamia msimamo wangu na kwenye akili yangu nilikua nikiwaza shida nilizonazo na namna gani nina njaa ya kufikia maisha yangu na kujitafutia kuinua na wengine,ninajua kwa hakika hilo haliwezekani nikiwa na wewe,na ndio maana nilikomalia msimamo wa kwamba mahusiano yetu hayapo. Naomba uniwie radhi sana,na wote niliowakosea kwa kauli yangu. Naamini nikipambana,nitafika na nitainua wengine kama ilivyo ndoto yangu. Ahsanteni.,"Heri Muziki katika akaunti yake ya Instagram |
No comments:
Post a Comment