Filamu yenyewe ilitoka mwaka 1983 chini ya Director T. Rama Rao na leading role ilisimamiwa na Hema Malini. Waigizaji kwenye filamu hii ni pamoja na Pran, Danny Denzongpa, Amrish Puri, Madan Puri na Prem Chopra,Amitabh Bachchan, Dharmendra wakiwa waigizaji waalikwa.
Stori yake.
Jan Nisar Akhtar Khan (Amitabh Bachchan) ni mfanyakzi katika hifadhi ya asili akiwa kama Afisa Misitu, anaishi na mkewe Zakhiya na mtoto wao wa kike Neelu. Siku moja akiwa katika majukumu yake walikuja wawindaji 3 ambao walikuwa wanakata miti kinyume cha utaratibu. Ram Gupta (Amrish Puri) anashawishi kumpa rushwa Khan ili waendelee na zoezi lao lakini anakataa. Walichokifanya wakampa kesi ya mauaji.
Alihukumiwa kwenda jela miaka 14 na huku nyuma mkewe pamoja na mtoto wake wanajiua
Miaka ya nyuma Vijay Singh alipotezewa familia yake mbele ya macho yake na Gupta hivyo akapanga kulipiza kisasi. Khan anakuja kugundua kuwa Gupta hakufa bali zilikuwa ni njama akaamua kufanya maamuzi ya kumuua eneo lile alilohukumiwa.
SOMA PIA: TUJIKUMBUSHE ALBAMU YA JUMA NATURE NAMNA ILIVYOWEKA REKODI
Kingine Vijay ana dada yake Miss Durga Singh ambae alijiunga na polisi kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa watu watatu lakini sheria ilikuwa ikipindishwa hivyo Khan akaamua kummaliza mmoja baada ya mwingine kwani alikuwa haamini kwenye sheria.
Filamu hii ilipigwa marufuku kwa muda nchini India kwani maudhui yake yalikuwa yakihamasisha watu wasiheshimu sheria zilizopo.
Lakini pia filamu hii wengi wanadhani Amitabh Bachchan alikuwa muhusiku mkuu (main character) kwani hata siku inazinduliwa posters zilibandikwa picha yake lakini yeye ni guest role.
Kingine cha kukumbuka kwenye filamu hii ni Wimbo wa Andhakanoon ambao ulipata umaarufu mkubwa.
No comments:
Post a Comment