Upo Hapo,Namna Ilivyounganisha Filamu Tatu Kali#Fahamu - teknomovies
Upo Hapo,Namna Ilivyounganisha Filamu Tatu Kali#Fahamu

Upo Hapo,Namna Ilivyounganisha Filamu Tatu Kali#Fahamu

Share This
Kama umetazama Kolabo la Wakali watatu,Mwana Fa,Ay pamoja na Fid Q hususani kama ulitazama Video basi utakuwa uliona namna kwanza Video ilivyoandaliwa ni kama Ulikuwa unatazama Filamu na Si muziki na pia utakuwa uliona namna Ambavyo kila mmoja alijipa jina lake Wengi hupenda kuita A.K.A.
Mwana Fa amejiita,The Godfather,Ay amejiita The Butcher huku Fid Q akijiita Lord Of War lakini je unajua chanzo cha majina hayo?
Ebu Tuone vyema chanzo cha majina Hayo Kama Ifuatavyo ambapo Tunaanza na Mwana Fa na Jina lake la The Godfather.
Hiyo Ni filamu kwanza inabidi ujue ambayo ilitoka mwezi Machi tarehe 24 mwaka 1972 ambapo kwa mwaka huo iliweza kuweka rekodi kadhaa mfano,Iliweza kuuza sana kuliko filamu zoote zilizoachiwa mwaka 1972 na pia iliweka rekodi Kadhaa kwa kipindi hicho kama kuwa ndio Filamu iliyouza zaidi kuzidi Filamu zoote zilizowahi kuachiwa chini ya mwaka 1972.

SOMA PIA:MASHABIKI WANATUCHEZEA SANA:AY

Ilitumia bajeti ndogo sana ya kiasi cha Dola milioni $7 lakini mauzo yaligonga mpaka Dola milioni $245.1.

Iliweza kuchukua Tuzo kadhaa kama Tuzo za Oscar kama Best Picture,Best Actor akichukua mtu mzima Brando na pia Best Adapted ScreenPlay Lakini pia ilikuwa kwenye zaidi ya vipengele 6.

Mafanikio ya Filamu hii,Mpaka sasa Kwa Marekani hutajwa kama Ndio Filamu Bora kwa upande wa Filamu zile za Kihuni (Gangster).

Baada ya Filamu hii kupata mafanikio zilikuja Zingine mbili ambapo nyingine iliachiwa Mwaka 1974 na ya tatu iliachiwa mwaka 1990.

Hivyo Mwana Fa kujiita The Godfather,Hata video ulipotazama utakuwa umepata picha kidogo kwa jinsi alivyoonekana kama Ganster flani hivi,Basi hata katika Filamu ndicho kilichokuwa hivyo Hivyo kama ungepata nafasi ya kutazama.

Ay-The Butcher
Hiyo nayo pia ni filamu Ya kutisha ambayo iliachiwa mwaka 2006,Haikuwa maarufu sana lakini kwa wanaopenda Filamu za kutisha basi lazima wataipenda hii na watakuwa wanaipata Fresh sana.

Vijana Kadhaa walikuwa wakisafiri kuelekea Las Vegas,Dogo ambae alikuwa akiendesha gari alikuwa mbabe sana na dharau sana kutokana na kwao walikuwa na pesa sana,Anaamua kufosi kupita njia ya mkato ambapo mbele kidogo wanapata ajali.

SOMA PIA:NATUMIA VYAKULA HIVI ILI SAUTI YANGU IWE NZITO:ENOCK BELLA

Mmoja wapo anafariki na gari lao kuharibika,Hivyo wanaamua kuchukua uamuzi wa kuomba msaada kwa nyumba ambayo wataikuta karibu,Katika kutembea huku na huku wanakutana na nyumba moja mbovu mbovu ambapo humo ndani wanakaa watu ambao kama hawana Akili fresh.

Ghafla wanaanza kufukuzwa na madogo kila anaekamatwa,Anageuzwa Nyama kama Namna jinsi Ay alivyokuwa anaichezea Nyama katika video basi ndo madogo ndicho walichogeuzwa(Haha!)

Fid Q :Lord Of War

Hii Filamu iliachiwa Mwaka 2005 ikifanywa na mkali Nicolas Cage pamoja na Ethan Hawke ambao walisimamia kazi Fresh.

Filamu hii iliangalia kupanda na kushuka kwa jamaa aliyefahamika kwa Jina la Yuri Orlov ambayo nafasi hiyo alicheza Nicholas Cage.

 SOMA PIA:DIAMOND ATAJA TAREHE YA UJIO WA ALBAMU YAKE MPYA

Inahusu nayo mambo ya kihuni huni,Lakini ikiwa imekaa kwenye ishu za madawa ya kulevya,Uuzwaji wa dawa za kulevya na mambo mengine ya hatari ambayo yalikuwa yakifanywa na Yuri.

Sasa kama uliona Fid Q jinsi alikava sehemu yake,katika video uliona kwa jinsi alivyokaa kama Bosi flani hivi mfano halisi wa Madoni wengi wanaofanyaga Biashara haramu.

Hapo ndipo unagundua kuwa pale watu wakali wanapokutana huwa hawafanyi Muziki tena bali wanafanya Filamu kama wao wenyewe walivyosema. 

Bonyeza Play Hapo Chini Kutazama Bonge La Filamu Yao.

                

No comments:

Post a Comment

Pages