Diamond Ataja Tarehe Ambayo Anaachia Albamu Yake,Pamoja na Singo Yake Na Rick Ross - teknomovies
Diamond Ataja Tarehe Ambayo Anaachia Albamu Yake,Pamoja na Singo Yake Na Rick Ross

Diamond Ataja Tarehe Ambayo Anaachia Albamu Yake,Pamoja na Singo Yake Na Rick Ross

Share This
Taarifa ikufikie Kwako wewe shabiki wa Diamond Platnumz,Ambapo leo ametangaza rasmi tarehe ya ujio wa Albamu yake pamoja na kutaja jina la singo yake na mkali Rick Ross mbayo anasema ametoka kufanya nae hivi karibuni.
 
Akihojiwa katika Studio za BBC,Na Mtangazaji Salim Kikeke Diamond Ametaja kuwa albamu yake ya A boy From Tandale ataiachia Desemba 01 mwaka huu.

Aliongeza Pia ngoma yake na Rick Ross ndiyo itayofuatia baada ya Hallelujah,Ambapo alitaja jina la wimbo huo ambao ameupa jina la Waka.

SOMA PIA:AMERICAN MADE,FILAMU KALI NA MKALI TOM CRUISE ICHUKUE SASA

"Nitaachia hiyo albamu sababu mimi kwa kila wiki narekodi nyimbo mbili,yaani lazima nizimalize nyimbo mbili kwahiyo nimejikuta nina nyimbo nyingi na nimeona ili zisipotee Mashabiki zangu inabidi wapate Albamu,"

Pia aliongeza kuwa Albamu hiyo kwake amepanga kuisambaza katika mfumo wa Ki digitali,katika mitandao mbalimbali ambako kwake anafikiri ndiko pesa ya sasa inaweza kupatikana kuliko kuuza katika mfumo wa Cds

SOMA PIA:MAMBO AMBAYO ULIKUWA HUYAJUI TOKA FILAMU YA TITANIC

"Lazima uangalie kwa sasa mahitaji ya watu,Wengi hawasikilizi Cds wanasikiliza sana kwenye Simu zao hivyo nipo kuiachia hii katika mfumo wa kimtandao zaidi,"
Mwezi Oktoba Diamond alipost Picha ya Cover ya Albamu yake hiyo katika mtandao wake wa Instagrama habari ambayo iliwashtua wengi hasa kutokana na Sasa soko la albamu kwa Bongo kufa na hivyo ujio wa Albamu hiyo inaweza kurudisha neema pia kwa wasanii wengi kuanza kuachia Albamu zao.

No comments:

Post a Comment

Pages