Mike Tyson arudishwa marekani baada ya kuzuiwa kuingia Chile. - teknomovies
Mike Tyson arudishwa marekani baada ya kuzuiwa kuingia Chile.

Mike Tyson arudishwa marekani baada ya kuzuiwa kuingia Chile.

Share This
Mike Tyson amezuiwa na mamlaka ya nchini Chile muda mfupi tu baada ya kutua uwanja wa ndege wa nchi hiyo kufuatia kutenda makosa ya jinai kipindi cha nyuma.

Tyson aliitwa nchini Chile kwa ajili uzinduzi wa channel ya Television (Local Televisison) lakini hakuwa na ruhusa ya kuingia katika nchi za Amerika ya kusini na hivyo kurudishwa Marekani.

Maafisa usalama wa Chile wamesema Tyson hakukidhi vigezo vya kuruhusiwa kuingia nchini humo kutokana na matukio aliyowahi kuyafanya kipindi cha nyuma.

Mbali na hilo waliamua kumsindikiza hadi uwanja wa ndege kisha kumpakiza kwenye ndege tayari kurudishwa Marekani.

Tyson alitumikia kifungo cha miaka 3 kati ya 6 alichohukumiwa mwaka 1990 kwa kosa la kubaka na pia matumizi ya dawa za kulevya (cocaine).

Mwaka 2013 pia alipata misukosuko ya kuruhusiwa kuingia London kutokana na matendo ya awali kama alivyofanyiwa Chile.

Sasa unaweza Kudownload Teknomovies App ili uwe wa kwanza kupata mastori, lakini pia usisahau Kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies kwa updates mbalimbali

No comments:

Post a Comment

Pages