Juma nature ni moja ya msanii aliechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa Bongo fleva ndani na nje ya nchi.
Katika orodha ya wasanii waliofanya makubwa kwenye muziki wa Bongo Fleva huwezi kuacha jina la Juma Nature. Nature ni mmoja wa wasanii anaejua kuimba na kurap tena anaweza kufanya vyote kwa pamoja kwa ufanisi mkubwa
Album yake ya kwanza aliitoa mwaka 2001 ilikwenda kwa jina la "Nini chanzo" na mwaka 2003 akatoa album yake ya pili ambayo imeweka historia ya kipekee kwenye ulingo wa burudani nchini. Album ya pili ilibatizwa jina la "Ugali" chini ya msimamizi P Funk Majani kutoka Bongo Record.
Uzinduzi wa Album hii ulifanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee na Nature alifanikiwa kujaza ukumbi huo hadi baadhi ya mashabiki kukosa nafasi ya kuingia ukumbini.
SOMA PIA: HERI MUZIKI AANDIKA WARAKA KUTHIBITISHA KUACHANA NA DIVA
Album ya Ugali ilibadilisha kabisa maisha ya Nature kimuziki na kiuchumi maana iliuza mauzo ya juu. Ingawa mpaka leo haijawekwa wazi ni nakala ngapi ziliuzwa, na kiasi gani cha pesa aliingiza vyote hivi vimebaki siri na vyote hivi vimesababishwa na mfumo mbovu wa usambazaji.
Katika Album hii kuna nyimbo kama Sitaki Demu, Ugali, Salio la Vesi, Jela, Aaah Wapi, Umoja wa Tanzania, Hali ngumu, Sitaki Demu RMX na Inaniuma Sana.
Nature ni moja ya wasanii wachache wanaoweza kufanya show kali bila ya kuwa na hit song mtaani.
No comments:
Post a Comment