1. Neno Samsung lina maana ya Nyota Tatu.
Nchini Korea neno Samsung kwa kiswahili ni nyota tatu, ndoto za mwanzilishi wa kampuni zilikuwa ni kuifanya kampuni ya Samsung kuwa kubwa na juu kama nyota na ndio maana logo ya kwanza ya Samsung ina alama ya nyota tatu.
Logo ya Kwanza Ya Samsung |
2. Logo ya Samsung imebadilishwa mara tatu
Ni kawaida kwa kampuni kufanya maboresho (innovation) ili kuweza kuwavutia wateja wake zaidi. Maboresho yanaweza kuwa ya kimuonekano wa bidhaa au logo. Kampuni nyingi hubadilisha logo mara kwa mara lakini hili limekuwa tofauti kwa kampuni ya Samsung kwani tangu kuanzishwa kwake mwaka 1938 wamebadilisha logo mara tatu tu. Logo inayotumika sasa ilianza kutumika mwaka 1993.
Logo Ya Sasa |
Logo Ya Kwanza |
Logo Ya Pili |
3. Bidhaa ya kwanza ya Kielektroniki kutoka Samsung ni TV
Kwa sasa Kampuni ya Samsung inajulikana kwa umahiri wao wa kutengeneza bidhaa za kielektroniki lakini zamani ilikuwa ni kampuni ya usindikaji wa vyakula, biashara ya nguo, bima na bidhaa zingine za rejareja. Kufikia mwaka 1960 kampuni hiyo iliingia kwenye biashara ya uuzaji wa vifaa vya kielektroniki na mwaka 1970 ikatoa bidhaa ya kwanza ambayo ni Tv.
4. Jengo refu kuliko yote la Burj Khalifa limejengwa na Samsung
Umeshtuka eeeh kusikia Samsung imejenga ghorofa...!!!! Sasa ni hivi Samsung ni kampuni ambayo ndani yake ina makampuni zaidi ya 80 ambayo yanafanya kazi mbalimbali ikiwemo kampuni ya Samsung C & T ambayo ndio ilikuwa mjenzi mkuu wa jengo hilo ingawa kulikuwa na makampuni mengine yaliyoshiriki katika ujenzi huo.
Burj Khalifa Jengo Refu Kuliko Yote Duniani |
5. Samsung ndio simu ya kwanza kutengeneza simu yenye mp3 player
Samsung ilifanikiwa kuwa wa kwanza kutengeneza mfumo wa mp3 kwenye simu hadi kufikia mwaka 2000 Samsung ilitoa simu ya Samsung SPH-M100 (UpRoar) ambayo ndio ilikuwa simu pekee kipindi hicho yenye uwezo wa kusoma file za MP3.
Simu Ya Kwanza Yenye Mp3 Player |
Ni hayo kutoka Samsung unaweza kuacha comment hapo chini kutujuza zaidi kuhusu kampuni hiyo na bidhaa zake kama Unajua zaidi.
No comments:
Post a Comment