FAHAMU :Mambo 5 kuhusu Kampuni ya Apple - teknomovies
FAHAMU :Mambo 5 kuhusu Kampuni ya Apple

FAHAMU :Mambo 5 kuhusu Kampuni ya Apple

Share This
Bidhaa kutoka kampuni ya Apple si ngeni machoni mwetu aidha kwa kuzitumia,kuzishika au hata kwa kuzisikia. Apple ni kampuni ya Tarakilishi (Computer) iliyoanzishwa mwaka 1976 na watu watatu ambao ni Steve Jobs, Steve Wozniak na Ronald Wayne.

Mwaka 2016 Kampuni hii ilitimiza miaka 40 tangu kuanzishwa kwake sasa yapo ambayo pengine huyafahamu kutoka kwenye kampuni ya Apple, mtandao wako Pendwa wa teknomovies.com umekuandalia machache kuhusu kampuni ya Apple.

1. Ronald Wayne ambae ni mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Apple aliuza hisa zake za Apple kwa dola 800 za kimarekani muda mfupi tu baada ya yeye na wenzie kuanzisha kampuni hiyo. Inasemekana kwamba alifanya hivyo baada ya kuhofia kwamba iwapo Apple wangeshindwa kibiashara basi mali zake zingebinafsishwa.
Ronald Wayne
Wasichojua wengi kuhusu Ronald Wayne ni kwamba anajihusisha na mahusiano ya jinsia moja na alimwambia habari hii Steve Jobs wakati bado wakiwa waajiriwa kabla hawajaanzisha kampuni ya Apple. Ronald anasema hajutii kuuza hisa zake wiki chache baada ya kuanzishwa, anadai kwamba alifanya maamuzi hayo kwa kutegemea taarifa aliyokuwa nayo kipindi kile. Yeye ndie mbunifu wa logo ya kwanza ya Apple.

2. Steve Jobs aliuza gari lake ili aweze kutengeneza kompyuta ya kwanza ya Apple 

Pesa ambazo ziligharamia utengenezwaji wa Komptyuta ya kwanza ya Apple ambayo ilikuwa inajulikana kwa jina la Apple Computer 1 ama Apple 1 zilitokana na pesa zilizokusanywa baada ya Steve Jobs kuuza usafiri wake wa pekee wa VW Mini Bus na Steve Wozniak kuuza calculator yake ya HP-65.
Jobs aliuza gari lake la pekee ili kulipa gharama za kutengeneza kompyuta ya kwanza. Gari hilo lilikuwa kama hili.

3. Kompyuta ya kwanza ya Apple ilichukua siku kumi tu 
Kompyuta ya kwanza ya Apple
Baada ya kuwa na pesa kwa ajili ya kutengeneza kompyuta iliwachukua siku kumi kukamilisha kazi. Kompyuta hiyo ikauzwa kwa dola za kimarekani 666.66. Wozniak anasema hakuwa anajua chochote kuhusu mambo ya kishetani kuhusishwa na namba hiyo kwa wakati kwa wakati huo hivyo hiyo namba haina uhusiano wowote na imani za kishetani.


4. Steve Jobs aliwahi kushushwa Cheo akaamua kwenda kuanzisha kampuni nyingine

Mwaka 1985 Steve Jobs alishushwa cheo cha umeneja na bodi ya wakurugenzi baada ya kutokea kugombea madaraka kati yake na aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa wakati huo. Jobs akaondoka na baadhi ya wafanyakazi wakaanzisha kampuni ya NEXT.

5. Apple walishawahi kuwa na pesa nyingi kushinda serikali ya Marekani 

Kwa kipindi cha mwaka 2011 Apple walikuwa wanahifadhi pesa kubwa kushinda hifadhi ya pesa za serikali ya Marekani, hii ilitokana na hasa na ukubwa wa madeni ya Marekani kwa wakati huo.

Bonus

Nakuongezea na hili. Ukiangalia kwa makini kwenye logo ya Apple kuna sura ya Steve Jobs.



Yako mambo mengi ambayo hayajulikani kwa watu hasa watumiaji wa bidhaa za Apple hayo matano ni machache ambayo mimi nimepata kuyafahamu.



No comments:

Post a Comment

Pages