FAHAMU APP ITAYOKUPATIA MASHAIRI ( LYRICS) KWA WIMBO WOWOTE UNAOSIKILIZA - teknomovies
FAHAMU APP ITAYOKUPATIA MASHAIRI ( LYRICS) KWA WIMBO WOWOTE UNAOSIKILIZA

FAHAMU APP ITAYOKUPATIA MASHAIRI ( LYRICS) KWA WIMBO WOWOTE UNAOSIKILIZA

Share This
Pengine unasikiliza Wimbo na unatamani pia uwe unaimba au uelewe maana yake zaidi lakini unashindwa kutokana na kutokujua vizuri Mashairi ya Wimbo Husika, Basi App hii itakufaa zaidi.

Ni mojawapo ya App maarufu sana Duniani, Inaitwa MusixMatch ambayo inakupa uwezo wa kupata Mashairi ya nyimbo mbalimbali, Tena pindi ambapo unasikiliza Wimbo husika huku ikikupa uwezo pia wa Kushare Mashairi hayo katika Sites mbalimbali.

SOMA PIA: REIGN OF ASSASSINS, WACHINA KATIKA FILAMU NDANI NI KICHAPO TU

MusixMatch ilianzishwa mwaka 2010, Na Waitaliano ambapo mpaka sasa ina Wafanyakazi 30 Tu, Huku ikikadiriwa kuwa na zaidi ya watumiaji Milioni 60, na Zaidi ya Mashairi ya nyimbo mbalimbali Milioni 14.
Ukiachana na kukupa uwezo wa kuona Mashairi lakini pia ni Player ambayo ina Muonekano mzuri ambao utakufanya uweze kusikiliza nyimbo mbalimbali katika Ubora mkubwa tofauti na App nyingine.

Umeipenda App hii Janja, Pakua HAPA sasa uweze kufurahia Huduma hiyo.

Note: App hii inafanya kazi kwa asilimia kubwa kwa Nyimbo za Kiingereza na kwa lugha nyingine pia lakini Mashairi ni machache sana tofauti na kiingereza Hivyo kwa Nyimbo za Lugha nyingine unaweza kupata ama Usipate.

No comments:

Post a Comment

Pages