Serikali Kugawa Kondomu Bure - teknomovies
Serikali Kugawa Kondomu Bure

Serikali Kugawa Kondomu Bure

Share This
Serikali imesema kuwa inatarajia kununua kondomu zitakazosambazwa nchi nzima bure kwa lengo la kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Neema Rusibamaila wakati wa uzinduzi wa mkakati wa kitaifa wa kondomu.
Dkt. Rusibamaila amesema kuwa kutakuwa na mashine maalumu zitakazofungwa kwenye maeneo ya sehemu za starehe kama Baa, Nyumba za kulala wageni, Migodini na katika kumbi za burudani ili kuweza kufanikisha zoezi hilo.
Hata hivyo, ameongeza kuwa Kondomu hizo zitanunuliwa kupitia fedha za Global Fund, ili kufikia malengo ya kupunguza maambukizi ya VVU ifikapo mwaka 2030.
Source : Dar24
Sasa unaweza Kudownload Teknomovies App ili uwe wa kwanza kupata mastori makali.

No comments:

Post a Comment

Pages