SpiderMan Mwakani Kuja Na Animation,Muhusika Sio Peter Paker - teknomovies
SpiderMan Mwakani Kuja Na Animation,Muhusika Sio Peter Paker

SpiderMan Mwakani Kuja Na Animation,Muhusika Sio Peter Paker

Share This
Marvel kwa sasa wanaamua kuja kivingine hasa baada ya kutangaza na kuachia Trailer ya Animation mpya ambayo imepewa jina la SpiderMan:Into The Spiderverse ambayo inatarajiwa kuachiwa Mwezi Desemba mwaka 2018 Tarehe 14.
Animation hiyo Tangu mwaka 2014 ilipangwa kuanza kufanyiwa kazi ikiwa ni baada ya taarifa hizo kuvuja katika mitandao mbalimbali na mwaka 2015 taarifa rasmi ilithibitishwa ambapo ikatangazwa kuwa filamu hiyo itaachiwa Mwezi July mwaka 2018 lakini kutokana na matatizo kadhaa wakati wa uandaaji Filamu hiyo ikasogezwa mbele.

Ujio wa Animation hii unatazamiwa kuwa wa kiutofauti sababu  muhusika atafahamika kwa jina la Miles Morales na sio tena Peter Paker.

Miles Morales Ni Nani?

Kama wewe ni mpenzi wa kufuatilia vijarida vinavyohusu Hawa SuperHeroes basi utakuwa unamjua ambapo huyu anakuwa SpiderMan wa pili baada ya Peter Paker kufariki katika Stori za vijarida.

SOMA PIA: FAHAMU FILAMU TANO KALI KWA MWAKA 2017

Alitokea kwa mara ya kwanza mwaka 2011, Na huyu kiasili ni Mweusi na Lengo kubwa la kumte ngeneza huyu ilikuwa ni kutokana na Inspiration kutoka kwa Rais wa kipindi hicho Barack Obama pamoja na mwigizaji Donald Glover hivyo Filamu hii itakuwa ya kwanza kutuonesha mhusika huyu Miles Morales.
Donald Glover

Vipi kwako umejipangaje kuipokea Filamu hii Mwakani?

Tazama Trailer Hapo Chini.          

No comments:

Post a Comment

Pages