List ya mastaa wanaomaliza mwaka 2017 wakiwa jela - teknomovies
List ya mastaa wanaomaliza mwaka 2017 wakiwa jela

List ya mastaa wanaomaliza mwaka 2017 wakiwa jela

Share This
Ni siku 37 zimesalia ili tumalize mwaka 2017. yapo mambo mengi yamejitokeza kwa mtu binafsi lakini pia kwenye ulimwengu wa burudani. teknomovies.com imekuandalia listi ya baadhi ya mastaa wanaomaliza mwaka 2017 wakiwa gerezani.

1. Joe Giudice ni moja ya mastaa ambao wanamaliza mwaka wakiwa gerezani. Ni mtangazaji wa vipindi vya TV na amekwenda gerezani kufuatia kukutwa na tuhuma za kusambaza ujumbe kwa njia ya email ambao ulikuwa wa uongo wenye lengo la kuwaibia watu. Wakati mpenzi wake Teresa amemaliza kifungo yeye nae anaendelea kutumikia kifungo miezi 41 gerezani. Jaji aliyetoa hukumu hiyo amesema ameamua kutoa adhabu kali kwa Joe kutokana na kuzuia kuwekwa hadharani thamani ya pesa zilizopo kwenye akaunti yake na mpenzi wake. Joe alihukumiwa March 2016
2. Suge Knight Mkurugenzi mwenza katika kampuni ya Death Row Records nae anamaliza mwaka katika mazingira ya Jela. Suge hayupo gerezani kwa sasa ingawa tayari amekutwa na hatia mbalimbali ikiwemo za unyang'anyi na kujaribu kuua. Kutokana na Tuhuma hizo kwa sasa anasubiri tu nyundo ya Hakimu kwani ameomba alipe $2.2 millioni ili aachiwe lakini imekataliwa na kesi inamalizwa January 2018 ingawa kwa sasa yupo nje.

3. C-Murder  Huyu ni kama lilivyo jina lake. Msela amehukumiwa jela kifungo cha maisha Gerezani kwa kosa la kumuua kijana wa miaka 16 mwaka 2002. C murder alipigana na kijana huyo aliyetambulika kwa jina la Steve Thomas wakati akitoka Club. Mbali na hukumu hiyo mwaka 2013 aliongezewa hukumu nyingine ya kulipa fidia kwa wazazi wa Steve ambapo alitakiwa alipe $ 1.1 millioni kama fidia.
4. Oscar Pistorius moja mtu ambae aliteka hisia za watu wengi wakati anahukumiwa kwenda jela kwa kosa kumuua mpenzi wake bila kukusudia. Mwaka 2012 Oscar alikuwa gumzo kila mahali kutokana na kutawala mashindano ya Olympic yaliyofanyika jijini London lakini mwaka mmoja baadae katika usiku wa Valentine (14 February 2013) akakumbana na kiunzi cha hatia ya kuua bila kukusudia  ambapo katika utetezi wake alisema kuwa alidhani ni majambazi wamevamia nyumbani kwake.


Mwaka 2014 mahakama nchini Afrika Kusini ikamtia hatiani rasmi ya kuua bila kukusudia na akahukumiwa kwenda jela miaka 5.

5. Meek Mill Pamoja na hukumu yake kupingwa na mastaa wengi kwa kuonekana kama ni ya kibaguzi lakini mwisho wa siku jamaa yuko nyuma ya nondo na atakaa huko kwa muda wa miaka 2 baada ya kukiuka masharti(probation) ambayo aliwekewa kutokana na kufanya makosa mwaka 2008 .

6. Elizabeth Michael "Lulu" Kutoka Bongoland mrembo Elizabeth Michael "Lulu" nae amechezea mvua ya miaka 2 gerezani kwa kosa la kuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake Steven Kanumba mwaka 2012. Atamaliza mwaka 2017 akiwa gerezani.

Tunawaombea wale wote wanaotumikia vifungo vyao kwenye magereza tofauti Mungu awape Afya njema na warejee uraiani wakiwa wapya kabisa, Ameen.






No comments:

Post a Comment

Pages