Kati Ya Pin Na Pattern Ipi Salama Zaidi?#Fahamu - teknomovies
Kati Ya Pin Na Pattern Ipi Salama Zaidi?#Fahamu

Kati Ya Pin Na Pattern Ipi Salama Zaidi?#Fahamu

Share This
Watumiaji wa Simu Janja (Smartphones) wengi ni kawaida kuweka Nywila(Passwords) katika Simu zao,Mara nyingi inaweza ikawa kwaajili ya Ulinzi kama lengo kuu la kuwa na Passwords lakini wengi wanaweza wakawa wanaweka Tu,Na imekuwa kama Utamaduni.
Kuna Passwords za aina nyingi kama Pattern,Kuweka Pin,Kutumia Kidole na sasa pia inayobamba ni ya Kuweka Sura.

Lakini Passwords maarufu ni za Pattern na na kuweka Pin Code Ambapo lengo kuu la makala hii ni kuonesha zipi ni Passwords nzuri zaidi kwa ulinzi wa simu yako kama ilivyoandikwa kutoka mtandao wa kiteknolojia wa Teknokona Ili kukufanya kujua ipi inafaa kwaajili ya kukupa ahueni pindi simu yako unapohisi haipo sehemu salama

Ios Vs Android

 Kwa watu wanaotumia na waliokuwa wanatumia Iphone katika hili watakuwa na ushahidi mzuri katika Loki ya simu za Iphone ambapo kwa mwanzo walikuwa wanatumia teknolojia ya Slide To Unlock ambapo Steve Jobs alisema kuwa aina hiyo ni nzuri kwa sababu,inazuia pindi hata simu ukiwa umeweka kwenye mfuko kushindwa kujibonyeza.

Lakini Pia Apple walikuwa na mfumo mwingine wa Passcode ambao mtumiaji alikuwa anaweka pin nne lakini kwa sasa hadi nane unaweza kuweka.

Android
Huku aina kubwa ya Loki inayotumika ni Pattern,ambapo kulingana na utafiti uliofanywa na Watafiti wa mambo ya Ulinzi na Usalama kutoka Marekani,Naval Academy pia wakishirikiana na Wataalamu kutoka chuo kikuu cha Maryland Bartimore County ambapo katika utafiti wao iligundulika ni rahisi zaidi kukalili Pattern za mtu anapofungua kuliko mtu anaetumia Pin katika ku Loki simu yake.
 Lakini ikumbukwe pia ni rahisi zaidi kwa mtu kufuatilia njia za mtu anazotumia kuweka Pattern lakini kwa Pin ni kazi kwa sababu mtu anakuwa anaruka ruka Tu.
 Hivyo Basi kama wewe ni mtumiaji wa Android fanya kubadilisha aina ya Loki yako,na uweke Pin ili uwe salama zaidi na hakikisha unatumia tarakimu sita na si nne.

Tuachie Pia maoni yako hapo chini kuhusu Hili.

Chanzo:Mtandao wa Teknokona pamoja na Picha. 




 

No comments:

Post a Comment

Pages